Pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bw. Hiiti Sillo
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mkutano na waandishi
wa habari katika kueleza maamuzi ya TFDA kufuta usajili na kubadili matumizi ya
baadhi ya dawa nchini. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa TFDA Makao Mkuu
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA)
imezifutia Usajili wa Dawa tano za Binadamu kutokana na kuwepo makosa
mbalimbali.
Hayo yameelewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi mkuu TFDA Bwana Hiiti
B.Sillo Wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo alisema
Mamlaka hiyo katika kupitia mifumo ya ufuatiliaji wa usalama na ubora wa
dawa nchini wamebaini uwepo wa dawa duni kwenye soko zenye madhara na zisizofaa
kwa matumizi ya Binadamu.
Mkurugenzi
Mkuu alieleza kuwa TFDA imefikia hatua ya kufuta usajili wa aina
tano za dawa za binadamu ambazo ni Dawa ya kutibu “Fungus” ya vidonge na
kapsuli aina ya ketocanazole kwa sababu
dawa hiyo inasababisha madhara hatarishi katika Ini kwa watumiaji.
Dawa nyingine ni ya kutibu malaria ikiwa katika mfumo wa maji na vidonge aina
ya Amodiaquine inapotumika yenyewe na
sababu ya kufutia usajili na kuzuia kuingia nchini ni kutokana na mabadiliko ya
mwongozo wa kisera wa kupima na kutibu malaria wa mwaka 2013 uliotolewa na
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, na kwamba ikitumika peke yake inaleta usugu
wa vimelea vya malaria.
Bw. Sillo aliitaja dawa nyingine ambayo ni hatari kwa matumizi ya binadamu
ni Dawa ya kutibu mafua na kikohozi ya Maji,Vidonge na Kapsuli zenye
kiambato hai aina ya Phenylpropanol amine ambacho anasema kinaleta madhara
hatarishi kwa binadamu kama vile kiharusi (Hemorrhagic sroke).
Mbali na hizo Dawa zengine ni Dawa ya kuua bacteria ya Sindano aina ya Chloramphenicol Sodiam Succinate
inayotengenezwa nchini India pamoja na dawa ya kuua Bakteria ya Maji na kapsuli
aina ya Cloxacillin ambazo zote kwa
pamoja Bw. Sillo alizitaja kwamba zina madhara kwa watumiaji ikiwemo kushindwa
kupumua na kupoteza Fahamu.
Katika Hatua Nyingine TFDA imebadili na kudhibiti zaidi matumizi ya aina nne za
dawa nchini. Mojawapo ni Dawa ya kutibu malaria aina ya vidonge yenye
mchanganyiko wa Sulphadoxine na Pyrimethamine (SP)ambayo imebadilishwa
kutoka kutibu malaria na kuwa kinga ya malaria kwa kina mama wajawazito kwa
mujibu wa mwongozo wa kisera wa kupima na kutibu Malaria wa mwaka 2013 wa
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Dawa nyingine zilizodhibitiwa zaidi
ni dawa aina ya Kanamycin Amikacin na Levofloxian kwa kuruhusu dawa hizi
kutumika kwa ajili ya ugonjwa wa kifua kikuu katika hospitali, vituo vya afya
na zahanati pekee. Bw. Sillo alieleza sababu ya kudhibiti zaidi ni kuzuia usugu
wa vimelea vya bacteria vya ugonjwa wa Kifua kikuu.
Aidha,
Bwana Sillo ametoa wito kwa wamiliki wa maduka ya Dawa pamoja wananchi
kuzingatia taarifa hizi za kiudhibiti kwa lengo la kuepuka madhara yanayoweza
kutokea kutokana na matumizi ya dawa hizo. Sillo alizitaka Hospitali mbalimbali
nchini pamoja maduka ya dawa kuaacha kuuza dawa hizo mara moja na kuzirudisha
walikozinunua kwa ajili ya kuziteketeza.
Tumeamka sasa! Hongera.
ReplyDelete