Mbunge wa Jimbo la Mvomero na Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla ameendelea na ziara Jimboni kwake kwa kutumia usafiri wa pikpiki,na safari hii ameweza kufika kijiji cha Sewe ambacho kipo kilomita 35 toka kijiji cha Maharaka.

Kutokana na kutokuwepo kwa barabara nzuri za kuelekea kwenye kijiji hicho,Mh. Makalla aliamua kutumia zaidi ya saa moja kufika kijiji cha Sewe kwa kutumia usafiri wa pikipiki ili mradi awafikie wananchi wake.

Mara baada ya kuwasili kijiji hicho,wananchi walifurahi na bila kujizua walimpomgeza kwa kuwajali kufika kijiji na kujionea changamoto zinazowakabili.

Amewahaidi kuendelea kushirikiana nao katika kukabiliana na changamoto zilizopo kijijini hapo na amechangia mifuko 50 kwa ajili ya ujenzi shule ya msingi kijiji kipya cha Sewe.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero na Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla akiwa safarini kwenda kijiji cha Sewe, kwa kutumia usafiri wa pikipiki. 

Mbunge wa Jimbo la Mvomero na Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla akiwa njiani kuelekea kwenye kijiji cha Sawe kilichopo kilometa 35 kutokea kijiji cha Maharaka,katika safari hiyo kuna baadhi ya maeneo alilazimika kushuka na kutembea kwa miguu kitokana na ubovu wa njia.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero na Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla akilakiwa na wananchi wa kijiji cha Sawe.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero na Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya vijana waendesha bodaboda waliofanikisha ziara yake hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...