KATIKA
kuhakikisha
kuwa 93.7 Efm inaendeleza utamaduni wake wa kushirikiana na wasikilizaji kama
familia, inatoa nafasi nyingine tena ya kuwawezesha kiuchumi kupitia shindano
lake la sakasaka ambalo limeanza rasmi jana Kigamboni jijini Dar es salaam.
Shindano hili linawawezesha washiriki ambao ni
wasikilizaji wote wa EFM, kujishindia zawadi ya fedha taslimu kuanzia
milioni moja na nusu, laki moja na shilingi elfu hamsini kwa lengo la kusonga
mbele na wasikilizaji wake kwa kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja kama shukrani pia ya kuwa wasikilizaji wetu.
Washindi wa shindano hilo wamegawanyika katika
maeneo matatu, ambapo kila wiki mshindi mmoja atajinyakulia kitita cha shilingi
milioni moja na nusu, washindi watatu wataondoka na laki moja kila mmoja na
wengine wanne watajinyakulia shilingi elfu hamsini kwa kila mmoja.
Hatua hii inakuja baada ya kituo hicho kuhitimisha
maadhimisho yake ya mwaka mmoja ambayo yalitoa gari mbili za biashara na
kuhitimishwa na Tamasha kubwa la miaka 16 ya msanii wa musiki wa kizazi kipya
Juma Nature, lakini pia kuwajazia mafuta wale wote wenye stika za efm katika
vyombo vyao vya usafiri ikiwemo boda boda, bajaji na gari.
“Kikubwa
zaidi ambacho tunakisisitiza kwa msikilizaji wetu kuwa hili shindano la sakasaka
linamlenga kila mtu anayesikiliza matangazo yetu kuanzia asubuhi hadi jioni
kila siku na jana tumeanza na wilaya ya Temeke ambayo itafuatiwa na Wilaya za
Ilala na Kinondoni” Amesema Dennis
Ssebo, Meneja Mahusiano na Mawasiliano machachari kabisa wa 93.7 wa EFM.
Mfumo
mzima wa shindano hilo unamtaka msikilizaji kufuatilia matangazo ya efm ili
kujua fedha hizo zimefichwa wapi ili aweze kujinyakulia vitita hivyo.
Kijana wa Temeke afurahia baada ya kusaka na kufanikiwa kupata mahela ya 93.7 EFM mwishoni mwa juma katika mambo ya Sakasaka
Zote hizi zangu kweli???
Sakasaka ikiendelea Temeke
Sakasaka hadi juu ya miti na kila kona....
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...