Familia ya marehemu Dr. Albert na Mwl Magdalena Chagula, tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa mapadre na paroko wa kanisa la Mt. Francis Xavery, Chang'ombe, wajane wote, ndugu, jamaa, marafiki na majirani wote walioshiriki nasi wakati wa msiba wa mpendwa mama yetu Mwl. Magdalena Chagula aliyefariki tarehe 24/6/2015.

Katika kumalizia msiba huu, tutakuwa na Misa jumamosi hii tarehe 8/8/2015 kanisani chang'ombe saa 2 kamili asubuhi na baada ya hapo tutaelekea Makaburini Kinondoni kwa ajili ya kupanda msalaba! Baadae tunawakaribisha wote nyumbani, chang'ombe maduka mawili kwa ajili ya kifungua kinywa. Wote mnakaribishwa.

Pia kutakuwa na misa ya shukrani katika kanisa la St.Ann's lililoko 120 First Ave, Toronto ON Canada kwenye corner ya Gerrard Street East na Degrassi saa kumi na moja jioni na baadae tafrija fupi kusherehekea maisha ya mama kwenye ukumbi wa kanisa.

Bwana ametoa na bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...