Tommorow ndio Kesho,raia wooote wa Instagram kukutana Sehemu moja tu Escape 1 kwenye Sikukuu yetu kubwa kabisa ya Instagram Party ikiwa na theme ya #BongoThrowBack mwendo wa Bongo fleva za miaka hiyo(Zile za kuamsha hisia na kukukumbusha matukio flani flani hivi) Usikose kukutana na uliemfollow,aliekufollow,Crush wako,Celebrities wa kipindi hicho na Sasa na watu kibao unaowakubali. Mtonyo ni 10,000 kawaida na 50,000 VIPz.📷📻🙌🏽
Mkurugenzi Mtendaji  wa Freconic ideaz, Fred Ngimba akifafanua jambo alipokuwa anaongea na waandishi wa habari jana katika fukwe za Escape One kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya tamasha kubwa la burudani litakalofanyika jumamosi hii  tarehe 28 ,kulia kwake ni Meneja mawasaliano wa Freconic ideaz Krantz Mwantepele 

Mmoja wa wadau akitembelea ukurasa wa INSTAGRAM  PART  TZ kupata taarifa mbalimbali kuhusu tamasha hili litakalowakumbusha wapenzi wa burudani nyimbo za zamani ,misemo ya zamani hata mavazi ya zamani kukiwa na kauli mbiu ya BONGO THROW BACK 

Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya Freconic Ideaz, imeandaa tamasha la burudani la ‘Instagram party’ litakalofanyika kesho kutwa kwenye Ukumbi wa Escape One Mikocheni jijini  Dar es Salaam likiwa na lengo la kuwakumbusha wapenzi wa muziki, mavazi na misemo ya kizamani.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa  Freconic Ideaz, Fred Ngimba alisema pia tamasha hilo litahusisha watu wenye ushawishi mkubwa katika mitandao ya kijamii na wasanii mbalimbali wa muziki na filamu wanamichezo na wanasiasa na kuweza kufanikisha mashabiki  wao kuweza kupiga nao picha katika red carpert.
Alisema wadau na marafiki mbalimbali wanaotumia mitandao ya kijamii watakutana siku hiyo kuweza kufahamiana na kubadilishana mawazo huku wakipata burudani mbalimbali.
“Kiingilio katika tamasha hili kitakuwa ni sh. 50,000 kwa viti maalumu na vile vya kawaida ni sh. 10,000, ambapo halitaishia hapa ila litaendelea katika Mikoa ya Mwanza, Morogoro, Tanga, Dodoma na Iringa,” alisema Ngimba.Alitoa mwito kwa wadau wa muziki wa mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi kushuhudia burudani itakayotolewa siku hiyo kwani kuna maboresho makubwa yamefanyika katika kuongeza ubunifu 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...