Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel(kulia)
akikabidhiwa kamusi kuu mpya ya Kiswahili kutoka kwa Katibu Mtendaji kutoka baraza la Kiswahili la
Taifa (BAKITA) Dkt Selemani Sewangi.Kamusi hiyo mpya ina jumla ya maneno makuu Zaidi ya elfu
thelathini na sita(36000) na kurasa 1264.
Katibu Mtendaji kutoka baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Dkt Selemani Sewangi(kushoto) akitoa
ufafanuzi kwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel
kwa baadhi ya maneno ambayo yapo katika kamusi mpya iliyotolewa na Baraza hilo leo jijini Dar es
Salaam.
www.oxfordictionaries.com Lugha ya Kingereza ina maneno 176,000 na ktk maneno hayo 47,000 ni maneno mfu a.k.a obsolete.
ReplyDeleteJe ktk maneno 36,000 ndani ya kamusi mpya ya BAKITA maneno mangapi hayatumiki .k.a mfu /obsolete?
Michuzi tunakutegemea utarudisha jibu toka BAKITA.
Mdau
Christos Papachristou
Diaspora