Na Maggid Mjengwa
Michango mingine ya fedha imetoka kwa wadau wa Mjengwablog kwa kutuma kwa njia ya simu. Siku ya Alhamisi niliongea kwenye Nuru FM na Ebony FM kuhusu wazo la mtandao huu kukusanya misaada kwa wahanga wa mafuriko Pawaga.
Mwitikio umekuwa wa kunishangaza hata mimi mwenyekiti wenu. Kwa fedha zilizochangwa taslimu na njia ya simu tumeweza hata kununulia magodoro 20. Miongoni mwa vilivyokusanywa kutoka kwa wana-Iringa wasamaria wema ni mahema 9 yenye ubora mkubwa.
Nimevutiwa pia na wanafunzi an viongozi wa Kimarekani kutoka Programu ya CIEE niliokutana nao majuzi ambao nao walipata taarifa hizo na wamechangia shilingi laki tatu fedha taslimu.
Hakika, mwitikio chanya ulilazimu utafutwe usafiri wa lori kwenda Pawaga hiyo kesho.
Shukran za pekee kabisa kwa kijana mwana-Iringa na mtaalamu wa masuala ya transport na logistics, Ahmed Salim ' Asas' ambaye amefanya jitihada za kuhakikisha vilivyokusanywa na wana-Iringa vinafika Pawaga leo. 
Mie leo nitakwenda Pawaga  na kwa vile viongozi wakuu wa Mkoa watakuwa Pawaga, basi, nitakabidhi misaada hiyo kwao ili nao wakabidhi kwa wahusika.
Shukran nyingi kwenu nyote mliounga mkono jitihada hizi na ambao bado mnaendelea kuchangia.
Kwa mwanadamu, kinachoangaliwa ni moyo wako, na si ukubwa wa unachotoa. Hata moyo wako ukiguswa tu kwa yaliyowapata ndugu zetu wa Pawaga ni faraja kwa walioathirika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...