Mbunge wa jimbo la Mafinga mjini Mhe. Cosato Chumi akiwasikiliza wafanyabiasha wadogowadogo
Sehemu ya wafanyabiasha wadogowadogo wakimsikiliza Mbunge wa jimbo la Mafinga mjini Mhe. Cosato Chumi.
Na Fredy Mgunda, Mafinga
Mvutano mkali kati ya wafanyabiashara wadogo wadogo mjini Mafinga mkoani Iringa na uongozi wa halmashauri hiyo umeendelea kufukuta baada ya wafanyabiashara hao kugomea kuondoka katika eneo la Mashujaa, wakidai maslahi ya watu wachache ndio yanayowahamisha katika eneo hilo jambo lililopelekea mbunge kuingilia kati .
Wakitoa kilio chao mbele ya mbunge wa mafinga mjini Mhe. Cosato Chumi wafanyabiashara hao walisema kuwa wamekuwa wakinyanyaswa kwa muda mrefu na halimashauri hiyo kwa kuhamishwahamishwa kila kuikicha na kupelekwa maeneo ambayo siyo rafiki kwa biashara zao .
Mwenyekiti wa wafanyabiashara hao Glibet Amoni alisema hapo awali walikuwa wakifanyia biashara zao pembeni ya soko la mafinga Uwanja wa mashuja ) na badaye kuja kuhamishwa katika eneo hilo na kupelekwa katika eneo la Kinyanambo ambalo pia halifai kwa biashara kwa kuwa kipindi cha mvua vitu vyao huzama kwenye maji kwa kuwa eneo hilo huwa linasimamisha maji pindi mvua inyeshapo .
Alisema kuwa baada ya kuona eneo hilo linaharibu biashara zao waliamua kurudi katika eneo lao la awali la mashujaa na kuutaarifu uongozi wa halimashauri hiyo kuwa wamerejea katika eneo hilo lakini walifanya biashara kwa majuma mawili na baadaye kuja kutangaziwa kuondoka katika eneo hilo na kwenda katika soko jipya ambalo pia miundombinu yake haijakamilika na wali sio eneo la wamachinga
Alisema kuwa walishanga kusikia matangazo ya barabarani kuwa hakutakuwa na mnada katika eneo hilo siku ya jumapili na walipoenda siku hiyo walikuta magari ya polisi yakiwa yametanda katika eneo hilo kuwazuia kufanya biashara jambo walilolalamikia kwa kuwa wengi wao wana mikopo katika maeneo mbalimbali na wanapaswa kurejesha mikopo hiyo
“Mheshimiwa mbunge wewe ndio msaada wetu kwani uliahidi kututetea sana na tunaona kuna mambo ya kisiasa yanaingia hapa kwani huyu mwenyekiti wa halmashauri Charles Makoga anatulazimisha kwenda kule kwa kuwa yeye anavibanda vyake kule sokoni ndio mana analazimisha tupelekwe kule na tunashangaa kuja kututangazia kibabe na kuondolewa a na polisi kama vile ni majambazi wakati ushuru wao tunalipa na eneo huwa tunafanya usafi kwani wanatufanyia hivii au sisi sio Watanzania?”
Waaliongeza kuwa wao siku yao ya kufanya biashara ni siku moja tu ya wiki yaani jumapili lakini wameshangaa kuona uongozi wa halimashauri hiyo kwa kushirikiana na wafanyabiashara wachache wa soko kuu wanaolalamika kutouza biadhaa zao pindi mnada huo unapofanyika katika eneo jambo ambalo siyo la kweli.
Akipokea kilio chao, Mhe Cosato chumi aliwataka wafanyabiashara hao kuwa wavumilivu kwani atakwenda kuzungumza na uongozi wa halmashauri hiyo ili kujua sababu za wao kutolewa katika eneo hilo na kupelekwa soko jipya eneo ambalo limetegwa kwa ajili ya soko na wala sio kwa ajili ya mnada wa siku moja .
Mhe Chumi alisema yeye kama mbunge hatakubali kuona wananchi wake wananyanyaswa na watu wachache kwani yeye ni mbunge wa watu wote na wala hatakubali kuona watu wake wakipelekwa katika maeneo ambayo siyo rafiki kwa biashara
‘’Kilio chenu nimekisikia na mimi nataka kukimbizana na kasi ya Magufuli ya kuwatetea wanyonge. Sioni sababu za msingi za nyie kuhamishiwa kule soko jipya wakati nyie huwa mnafanya mnada kwa siku moja tu.
"Hao wanaosema hawauzi kwanini wanakuwa wabinafsi hivyo. Yaani wao wanauza kwa siku sita nyie mnada wenu ni siku moja halafu eti wanasemna hawauzi mi niwambie waache ubinafsi na hili sitakubaliana nao..." alisema.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...