Na Zuena Msuya
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesaini
kibali cha kuhamisha leseni ya uchimbaji wa kati  wa madini kutoka
ampuni ya uchimbaji wa madini ya China ya Henan AfroAsia  Geo-
Engeneering ( Tanzania) kwenda Kampuni ya uchimbaji wa Dhahabu
ZEM Tanzania Limited.
Akizungumza mara baada ya kusaini kibali hicho leo, jijini Dar es
salaam,Profesa Muhongo amesema kampuni hiyo itaanza shughuli za
uchimbaji mwanzoni mwa mwezi Desemba mwaka huu 2016, katika
ijiji cha Nyasirori wilayani Butiama Mkoani Mara.
Alifafanua kuwa kusaini kwa kibali hicho kunatoa fursa kwa kampuni
ya china ya uchimbaji wa madini ya ZEM,ambayo iliingia
makubalianao ya kufanya kazi na kampuni ya Henan AfroAsia  Geo-
Engeneering ( Tanzania) mwezi Desemba mwaka 2015.
Gharama za mradi huo zinakadiriwa kufikia kiasi cha dolla za
Marekani mlioni43.3. 
 Waziri wa Nishati Profesa Sospeter Muhongo akisaini kibali cha
kuhamisha leseni ya uchimbaji wa kati  wa madini kutoka
Kampuni ya uchimbaji wa madini ya China ya Henan AfroAsia
Geo- Engeneering ( Tanzania) kwenda Kampuni ya uchimbaji wa
Dhahabu ZEM Tanzania Limited, tukio lililofanyika katika ukumbi
wa mikutano wa Wizara ya Nishati na Madini 
 Kansela wa ubalozi wa China, Gou Haodong(kushoto) akiweka saini
kitabu cha wageni ofisi kwa Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa
Nishati Profesa Sospeter Muhongo(kulia) mara baada ya kumaliza
kutano wao.
 Waziri wa Nishati Profesa Sospeter Muhongo( wa pili kulia), Kansela
wa ubalozi wa China, Gou Haodong(wa pili kushoto) na  Maneja wa
ampuni ya uchimbaji madini ya Henan AfroAsia Zhang Jiangbo kwa
pamoja wakionesha kibali cha kuhamisha leseni ya uchimbaji wa
kati  wa madini kutoka Kampuni ya uchimbaji wa madini ya China
ya Henan AfroAsia  Geo- Engeneering ( Tanzania) kwenda
Kampunia uchimbaji wa Dhahabu ZEM Tanzania
Limited,uchimbaji wa madini hayo utafanyika katika kijiji cha
Nyasirori Wilayani Butiama Mkoani Mara kuanzia mwezi Desemba
mwaka 2016.
 Waziri wa Nishati Profesa Sospeter Muhongo ( wa pili kulia),
Wakibadilishana mawazo na Kansela wa ubalozi wa China, Gou
Haodong(wa pili kushoto) katika Ofisi ya Waziri wa Nishati na
Madini baada ya kumaliza kusaini kibali cha kuhamisha leseni
chimbaji wa madini katika kijiji cha Nyasirori wilayani
Butiama utakaoanza mwezi Desemba mwaka huo, Maneja wa
Kampuni ya uchimbaji madini ya Henan AfroAsia
Zhang Jiangbo(kulia)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...