Benki ya TIB Corporate imepongezwa na wadau mbalimbali juu ya mpango wake wa kuwawezesha kifedha makandarasi wa ndani ili waweze kutekeleza vema majukumu yao ya kikandarasi.

Akizungumza wakati wa mkutano wa mashauriano wa mwaka wa bodi ya makandarasi, Kaimu Msajili wa Bodi ya Makandarasi nchini (CRB), Rhoben Nkori alisema anaipongeza benki ya TIB Corporate kwa kukubali kuwapa makandarasi mikopo na udhamini bila gharama zozote kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali.

‘Bodi ya Makandarasi (CRB) imeingia makubalinao na benki ya TIB Corporate ili iweze kutoa mikopo baada tu ya kupata barua kutoka bodi ya makandarasi’ alisema bwana Nkori.Mkutano huo wa mashauriano na maonyesho wa bodi ya makandarasi mwaka huu una dhima ya, ‘Mpango wa makusudi wa kuwajengea uwezo wa kiuchumi endelevu wakandarasi wazalendo, Changamoto na mustakabali wake’.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TIB Corporate, Frank Nyabundege amesema kama benki inayomilikiwa na serikali inaunga mkono moja kwa moja juhudi za serikali za kuwawezesha makandarasi ili waweze kushiriki katika kukuza uchumi.

‘Tumeona juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuwawezesha wakandarasi wazalendo, kwa kuanza kuwapa miradi mikubwa, ndio maana tumeanzisha huduma mbalimbali za kibenki kama dhamana ya kibenki bila gharama yoyote pamoja na mkopo wa ununuzi wa vifaa ambazo zitawasaidia wakandarasi wa ndani kufanikisha miradi yao bila usumbufu wowote’ alisema bwana Nyabundege.
Rais John Pombe Magufuli akimkabidhi cheti cha pongezi kwa kudhamini mkutano bodi ya makandarasi nchini, Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya TIB Corporate, Fank Nyabundege. Anayetazama kati kati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Makandarasi (CRB) Eng. Consolata Ngimbwa akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. 
Mkuu wa Kitengo cha Mauzo ya Mikopo wa Benki ya TIB Corporate, Theresia Soka akimweleza mmoja wa makandarasi kuhusu huduma zinazotolewa na benki yake. Anayetazama kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa benki ya TIB Corporate, Bahati Minja.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...