Waendesha pikipiki zipakiazo abiria jijini Dar (Bodaboda) usiku huu wamefunga Barabara ya Mandela eneo la Riverside, Ubungo kwa kupanga mawe na kuegesha pikipiki zao, baada ya mwenzao mmoja kugongwa na gari ambayo ilitoweka eneo la tukio. Wamedai kuwa wameamua kuchukua uamuzi huo wa kafunga Barabara hiyo, kwa kuwa wamekuwa wakidharauliwa na watu wenye magari, hivyo wamechukua uamuzi huo kushinikiza na wao kuheshimiwa kama vyombo zingine vya usafiri.
Home
Unlabelled
Breaking nyuzzzz....: Bodaboda wafunga Barabara ya Mandela usiku huu baada ya mwenzao kugongwa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Nchi ya WAGARATIA NANI ALIWALONGA? Kila mtu anashika sheria mikononi?
ReplyDeleteDawa kuwapiga chini maeneo ya mjini. Ndumu, viroba na vyombo vya usafiri wapi na wapi???!!
ReplyDeleteUjinga kama huu ukiruhusiwa kuendelea ama kuvumiliwa ndio hufanya nchi zisitawalike. Break down ya law and order kwenye nchi inaaanza kidogo kidogo. Waulize Kenya.
ReplyDeleteKuendelea kuwalea bodaboda kwa sababu zozote zile kutakuja kuleta maafa makubwa siku zijazo, kwani tabia ya kuhisi kudharauliwa iko kwa kila mtu ajionaye dhaifu kwa mwingine, hata madereva wa magari madogo hujiona vivyo hivyo kwa wale wa magari makubwa au mabasi na wa mabasi hujiona hivyo hivyo kwa wale wa malori makubwa, lakini hujawahi kuona akigongwa ajionaye dhaifu wengine wenye vyombo kama chake wakiamua kuchukua sheria mkononi. hii himaya ya muungano usio rasmi wa watu wa aina fulani wenye kujimilikisha maamuzi ya kisheria dhidi ya wengine ikiachwa iendelee itazaa kundi ambalo linaweza kuwa hasi, si kwa wengine tu, bali hata kwa serikali na vyombo vyake vya dola, ni muhimu na ni lazima nguvu ya ziada itumike kuzuia na kukomesha kabisa mawazo haya, kwani tunajiundia bomu lisubirilo kulipuka kwa kishindo na kusababisha maafa yasiyokifani
ReplyDelete