Mteja akipata huduma katika duka la Tahfif lililopo katika mtaa wa Mansfield  jijini Dar es Salaam. 
 Mteja akipata huduma katika duka la Tahfif.
 Wafanyakazi wa duka la vifaa vya elimu la Tahfif wakiwa kazini.
 Baadhi ya vifaa vya elimu.
 Wafanyakazi wa duka la Tahfif wakiwa katika picha ya pamoja.


Na Maria Inviolata
“Lengo la kuuza vifaa vya shule kwa bei rahisi ni kutoa mchango wetu katika elimu kwa kuwauzia wateja wetu vifaa hivyo kwa bei nafuu ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi nchini” ni kauli ya Mkurugenzi wa duka  la vifaa vya shule na ofisini la Tahfif, Mohamed Merali.

Kwa kuthibitisha kauli yake Merali anafafanua kwa lugha ya Kiarabu neno Tahfif maana yake ni “Rahisi”. Duka hilo linajihusisha zaidi na kuuza vifaa vya shule, ofisini, vifaa vya kompyuta na vifaa vya watu wenye ulemavu wa macho.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Mkurugenzi huyo anasema kuwa Tahfif ilianzishwa  kwenye miaka ya 1972 na baba yao na kukabidhi duka hilo mikononi mwa wanafamilia ili kuundeleza adhma yake ya kusaidia elimu nchini, wakisimamiwa na hayati Jargis Merali, ambaye alibuni mpango mwingine wa kudhamini burudani na michezo.

Awali duka hilo lilikuwa maeneo ya Kariakoo tu, kwa juhudi za wanafamilia hao kuenzi kauli ya baba yao ya kuchangia elimu wakafungua duka lingine katikati ya jiji maeneo ya Posta.

Mwandishi wa makala hii alipotaka kujua siri ya kuuza vifaa vya elimu kwa bei rahisi kama haiathiri biashara hiyo au labda kuna njia nyingine  mbadala inayofidia gharama hizo, Mohamed anasema kuwa siri yao kuu ni kuuza kwa urahisi vitu vingi kwa muda mfupi na kuagiza vingine, kwani ukiuza kwa bei kubwa itakugharimu muda mrefu kumalizia bidhaa zako zilizo sokoni.
Mkurugenzi huyo anasema kuwa ukiwa makini na faida ambayo kwa macho ya wengi inaoneka ni kidogo, lakini kwa wao ni faida inayojitosheleza kabisa.
Mwandishi alipouliza inakuwaje  baadhi ya wateja wa Tahfif wa bidhaa za jumla wanauza ghali bidhaa hizo kwenye maduka yao, Mkurugenzi huyo anatoa wito kwa wateja hao kutoongeza sana bei, kwani jambo hilo linawaumiza wazazi walio wengi kwa kushindwa kununua mahitaji ya vifaa vya shule, ingawa kibiashara faida inatakiwa ili kulipa gharama na lengo la kibiashara, lakini kwa mfanya biashara makini haitaji kuweka bei ya juu katika biashara zake, jambo hilo linawaathiri wateja wake kwa njia nyingi.
Mkurugenzi huyo anatoa wito kwa wateja wake wenye maduka ya vifaa vya shule na ofisini, kuuza vifaa hivyo kwa bei ambayo haiwaumizi wateja, lengo  kuu liwe ni pamoja na kusaidia wanafunzi ili wapate vifaa shule kwa urahisi, kwani jambo hilo litasaidia kuinua elimu nchini.

Mteja wa duka hilo wa muda mrefu ambaye hakutaka jina lake litajwe, anasema kuwa alianza kununua vifaa vya shule tangu mwanae akiwa darasa la Kwanza hadi sasa ambapo mtoto huyo yupo Kidato cha Tatu, mteja huyo anatoa shukrani kwa duka hilo kwa kuuza vifaa hivyo kwa bei nafuu  na jirani yake aliyemuelekeza ilipo Tahfif, naye mteja mwingine Joseph Mwalugenge anasema kuwa  yeye ananunua vifaa hivyo dukani hapo kwa sababu mahitaji yake yote yanapatikana hapo. 

Mteja mwingine wa muda mrefu dukani hapo, anasema inambidi kutoka Kigamboni ili kukidhi mahitaji yake ya kupata vifaa hivyo hapo Tahfif.
Hivi sasa Tahfif inatoa huduma ya kuuza vifaa vya watu wenye ulemavu wa macho, kama vile Kompyuta maalum na vifaa vyote vya kisasa vinavyohitajika watu hao.
Tahfif inaagiza bidhaa zake kutoka katika nchi za China, Dubai na India, licha ya kuuza vifaa vya elimu kwa bei rahisi, Tahfif hutoa misaada mbalimbali kwa watoto na watu wenye uhitaji kama vile kwenye vituo vya kulelea watoto yatima nakadhalika.
Lengo kuu la maduka ya Tahfif ni kuendelea kutoa huduma ya kuuza vifaa vya kisasa zaidi vya Shule na  Ofisini ili kukidhi mahitaji ya Wanafunzi kwa kuinua elimu nchini, pia kutoa udhamini wa michezo na burudani kwa lengo la kuzalisha wanamichezo bora, anasema Mohamed Merali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hili Duka kwa kweli ni la zamani sana, nakumbuka lilikuwa Kariakoo mkabala na soko kuu la Kariakoo, kwa kweli vifaa bora na kwa bei nafuu (takhfif) kimbilio letu by that time lilikuwa ni hapo. Kwa kweli imefanya nikumbuke mbali arround 80's

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...