Kikosi cha wachezaji na viongozi 24 wa timu ya taifa, Taifa Stars, kimewasili jijini Nairobi leo Ijumaa asubuhi kwa ajili ya mechi ya kirafiki na timu ya taifa ya Kenya, Harambe Stars, itakayochezwa Jumapili, Mei 29 kwenye uwanja wa Safaricom Kasarani.
Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. John Haule, amewatembelea wachezaji hao na viongozi wao kwenye hoteli ya Nairobi Safari Club walikofikia na kuwatakia matayarisho mema na ushindi watakapocheza na Harambee. Aliwahakikishia kuwa hali ya usalama jijini Nairobi imethibitiwa.
 Balozi Haule akiongea na Wachezaji wa timu ya Taifa. Kulia ni Kocha Mkuu Boniface Mkwasa na wa pili kushoto ni Mshauri wa timu Abdallah 'King' Kibadeni. 
 Wachezaji wa Taifa Stars wakimsikiliza Balozi Haule.
Balozi Haule katika picha ya pamoja na wachezaji na viongozi wa Stars

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...