Taasisi ya Vodacom Foundation Tanzania itaendelea kusaidia wasichana nchini kuondokana na vikwazo vinavyosaabisha wabaki nyuma pia kutojiamini kupitia mradi wake wa ‘Hakuna Wasichoweza’ ambao imeanza kuutekeleza mkoani Mtwara.

Mradi huo ambao inautekeleza kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la T-MARC Tanzania na wadau wengine umelenga kuwapatia wasichana waliopo mashuleni elimu ya afya ya uzazi ikiwemo kuwapatia vifaa vya kuwaweka salama wanapokuwa kwenye vipindi vya hedhi.

Akiongea wakati wa maadhimisho ya siku ya hedhi duniani yaliyofanyika mwishoni mwa wiki,Mkuu wa Vodacom Tanzania Foundation,Renatus Rwehikiza,alisema wataendelea na kampeni ya kukabiliana na changamoto za hedhi na alishauri kuwa  jukumu hili sio la serikali pekee bali linahusu taasisi zote na watu binafsi wa kuwa linachangia watoto wa kike hasa wanaotoka kwenye familia zenye vipato vya chini kubaki nyuma na kukosa kujiamini.

“Vodacom Foundation siku hii  ya hedhi duniani ni muhimu kwetu kwa kuwa tayari kupitia mradi wetu wa ‘Hakuna wasichoweza’  tumeanza kusaidia wasichana kukabiliana na changamoto wanazozipata wanapokuwa kwenye hedhi mojawapo ikiwa ni kutohudhuria masomo katika vipindi hivyo kutokana na kutokuwa na  vifaa vya kuwaweka salama na miundo mbinu isiyo rafiki kwenye shule wanazosomea,na mafanikio makubwa yameanza kupatikana na tunatamani miradi kama hii itekelezwe nchi nzima”.Alisema Rwehikiza.

Alisema ukosefu wa miundo mbinu rafiki kwa watoto wa kike mashuleni ya kuwaweka salama wanapokuwa kwenye hedhi nchini ni tatizo kubwa ambalo sio la kufumbia macho bali linahitaji mikakati maalumu ya kulimaliza kwa kuwa linarudisha nyuma maendeleo ya wasichana  kielimu ambapo ipo idadi kubwa ya wasichana hawahudhurii masomo kwenye vipindi vya hedhi.

Meneja Mradi huo kutoka  taasisi ya T-MARC Tanzania inayotekeleza mradi chini ya  ufadhili wa USAID na Vodacom Foundation,Lilian Semanyesa, amesema kuwa mradi umeonyesha kuwa na mafanikio ambapo hadi kufikia sasa idadi kubwa ya wasichana wamepata mafunzo ya afya ya uzazi  na pedi za bure  kuwafikia wasichana  waliopo mashuleni na wasiokuwa mashuleni mkoani Mtwara.

“Lengo la Mradi wa Hakuna Wasichoweza  ni kuwapatia elimu ya uzazi,afya,kuwajengea uwezo wa kujiamini na kuwapatia Pedi watoto wa kike zaidi ya wasichana 10,000 waliopo katika umri wa kuvunja ungo katika mikoa ya Mtwara na Lindi.Mradi unatekeleza mpango wa taifa kwa vitendo wa kuhakikisha watoto wa kike hawabaki nyuma bali wanapata fursa sawa na wenzao wa kiume”.Alisema
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi, akisalimiana na Meneja ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Foundation, Sandra Osward, wakati wa maadhimisho ya siku ya Hedhi Salama iliyofanyika katik viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa mradi wa Hakuna wasichoweza wa T-Marc, Lilian Semanyesa na Meneja ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Foundation, Sandra Osward, (wapili kulia) wakitoa maelekezo kwa wanafunzi wa shule ya msingi ya Dareda Mission iliyopo Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara, walipotembelea banda la Vodacom Foundation na T-Marc Tanzania wakati wa maadhimisho ya siku ya Hedhi Salama iliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam jana, Mifuko hiyo ni wadau wakubwa wa kutoa elimu mashuleni kwa wasichana ya jinsi kujisitiri.
Baadhi ya wanafunzi washule za sekondari wakipatiwa elimu juu ya matumizi ya pedi na Meneja ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Foundation ,Sandra Osward, wakati walipotembelea banda la T-Marc Tanzania na Vodacom Foundation wakati wa maadhimisho ya siku ya Hedhi salama iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana,Mifuko hii ni wadau wakubwa wa kutoa elimu mashuleni kwa wasichana ya jinsi kujisitiri kupitia mradi wao wa "Hakuna wasichoweza".

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...