Na  Abel Daud wa 
 Globu ya Jamii, Kigoma
ASKOFU Mkuu wa kanisa la Anglika Tanzania Mhashamu Dr.Jacob Chimeledya amewataka waumini wa kanisa la Anglikana pamoja na watanzania wote kuwajibika kufanya kazi kwa bidii ili kuondokana na hali ya utegemezi katika familia pamoja na kukuza uchumi wa taifa.

Hayo ameyasema wakati alipokuwa akizindua kanisa la anglikana la Mt.PETRO,Parish ya Katubuka katika DIOCESE YA MAGHARIBI MWA TANZANIA(DWT) mjini Kigoma ambapo amesisitiza kwa nguvu ju ya kufanya kazi kwa ufanisi pasipo kuweka uzembe katika kazi.
Aidha akitoa mfano kwa waumini wa kanisa hilo askofu Jacob amepanda mti wa kumbukumbu kanisani hapo kama kiashiria kuwa lazima kila mtanzania awekeze katika misitu kwani kupitia misitu,ndani yake hupatikana faida kadha wa kadha ambazo Watanzania watanufaika nazo.
Pamoja na hayo ameitaka serikali kupunguza ghalama za mitungi ya gesi na kukopesha kila mfanya kazi wa Tanzania na Watanzania kwa ujumla ili kuondokana na uharibifu wa misitu.
Hata hivyo aliongeza kuwa ni lazima sasa kila mtu afanye kazi kwa bidii ili kuondokana na hali ambayo imezoeleka ya Watanzania kuwa wapokeajia tu,pasipo kujali dini wala chama cha siasa na kuendana na kauli mbiu ya hapa kazi tu ya raisi wa awamu ya tano.

 ASKOFU Mkuu wa kanisa la Anglika Tanzania Mhashamu Dr.Jacob Chimeledya akizindua kanisa la Anglikana la Mt.PETRO,Parish ya Katubuka katika DIOCESE YA MAGHARIBI MWA TANZANIA(DWT) mjini Kigoma.
  ASKOFU Mkuu wa kanisa la Anglika Tanzania Mhashamu Dr.Jacob Chimeledya akipanda mti baada ya kukizindua kanisa la Anglikana la Mt.PETRO,Parish ya Katubuka katika DIOCESE YA MAGHARIBI MWA TANZANIA(DWT) mjini kigoma
 ASKOFU Mkuu wa kanisa la Anglika Tanzania Mhashamu Dr.Jacob Chimeledya akikata utepe kufungua rasmi kanisa la Anglikana la Mt.PETRO,Parish ya Katubuka katika DIOCESE YA MAGHARIBI MWA TANZANIA(DWT) mjini Kigoma. Picha na Abel Daud wa Glou ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...