Shirika la nyumba la Taifa (NHC)limekabidhi nyumba za makazi kumi kwa banki kuu ya Tanzania(BoT) ikiwa ni sehemu ya nyumba walizozinunua katika mradi wa eneo la Shangani ambao katika utekelezaji wa ujenzi huo wameingia mkataba na Bancabc katika ununuzi wa nyumba hizo.

Mkurugenzi mkuu wa NHC,Nehemia Mchechu alisema hadi kukamilika kwa mradi huo utagharimu kiasi cha Sh 4.8 bilioni ambapo una majengo matatu yenye ghorofa tano kila moja ambapo kwa ghorofa zote zina nyumba za kuishi 30 zenye vyumba vitatu kila moja huku banki kuu wakiwa tayari wamenunua jengo mojalenye nyumba kumi.

“Nyumba hizi zinauzwa kwa wananchi, hadi hivi sasa benki kuu imenunua ghorofa moja yenye nyumba kumi za makazi ambapo kila moja ina vyumba vitatu vya kulala viwili vikijitegemea,jiko la kisasa lenye stoo,sebule ,sehemu ya chakula na stoo ya ziada na sehemu na kuogea na mita za maji na umeme,”alisema Mchechu

Aidha alisema shirika hilo lina mradi mwingine eneo la Raha Leo ambao pia wameingia mkataba na Bancabc ambayo imetoa fedha kwa ajili ya kufanikisha mradi huo ambao utagharimu kiasi cha 22.5 bilioni hadi kukamilika ambapo Benki kuu tayari imenunua majengo mawili yenye nyumba 40 kwaajili ya wafanyakazi watakaokuwa Mtwara.

Mkurugenzi wa masoko kitengo cha makampuni makubwa kutoka Bancabc,Khalifa Zidadu alisema NHC ni moja ya wateja wao ambao hushiriki kuwasapoti katika miradi yao ikiwa ni moja sehemu ya utendaji kazi wao.

“NHC ni moja ya wateja wetu ambao tumeshiriki katika kuwasapoti kwenye miradi miwili wa Shangani ambao tumewaunga mkono kwa asilimia 30 na mradi wa Raha Leo tumewapatia kiasi cha 11 bilioni ili kuufanikisha na hii ni sehemu ya utendaji kazi wetu,”alisema Zidadu.


Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akimkabidhi ufunguo
Gavana wa Benki kuu ya Tanzania- B0T Prof. Benno Ndulu

Gavana wa Benki kuu ya Tanzania- BoT Prof. Benno Ndulu akimsikiliza mkurugenzi wa masoko kitengo cha makampuni makubwa wa Bancabc Khilifa Zidadu wakati wa uzinduzi wa nyumba za BoT Mtwara na kushoto kwa gavana ni Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu.
Gavana wa Benki kuu ya Tanzania- BoT Prof. Benno Ndulu akifafanua jambo kuhusina na ununuzi wa nyumba kwa ajili ya wafanyakazi wa benki hiyo mkoani mtwara, kulia kwa gavana ni mkurugenzi wa masoko kitengo cha makumpuni makubwa wa Bancabc Khalifa Zidadu na kushoto kwa gavana ni Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akitoa maelezo ya kukamilika kwa mradi wa nyumba kwa ajili ya wafanyakazi wa benki kuu ya tanzania mkoani mtwa kwa gavana wa benki hiyo Prof  Benno ndulu na Mkurugenzi wa masoko kitengo cha makampuni makubwa wa Bancabc Khalifa Zidadu.
Gavana wa Benki kuu ya Tanzania- BoT Prof. Benno Ndulu akimshukuru Mkurugenzi wa masoko kitengo cha makampuni makubwa wa Bancabc Khalifa Zidadu kwa kuwezesha BoT kununua nyumba hizo mkoani Mtwara, kushoto  ni Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 25, 2016

    Mbona moyo ulishtuka nilipoona hizi picha. Nilifikiri ze fulanas imefufuka

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...