Mwanamuziki wa Kimataifa wa Miondoko ya Dansi kutoka Nchini Congo, Antoine Christophe Agbepa Mumba maarufu kama "Koffi Olomide" amehukumiwa kifungo cha miezi 18 jela baada ya kuonekana na hatia ya kumdhalilisha kwa kumpiga dansa wake wakati wakiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Nchini Kenya hivi karibini.

Mwanamuziki huyo alikamatwa mapema leo akiwa nyumbani kwake katika mji wa Kinshasa na kupelekwa Mahakamani moja kwa moja na kukutwa na hatia hiyo.

Hukumu hiyo imetolewa baada ya ushahidi huo kuonekana akimpiga dansa wake na atatakiwa kuitumikia adhabu hiyo kwani hajapewa nafasi ya kulipa faini ya aina yoyote ile.

hatua ya kumkamata Mwanamuziki huyo ilifikiwa baada ya kuanzishwa kwa kampeni ya baadhi ya wadau wa maswala ya kijamii wakiongozwa na Zakarie Bababaswe aliyefungua kesi kwa niaba ya Serikali ikiwa ni madai ya udhalilishaji kwa dansa wake, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Kongo, kuamua kukamatwa kwake na kusema anataka haki itendeke.

CHINI NI VIDEO INAYOONYESHA TUKIO HILO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 27, 2016

    Hii taarifa si sahihi,Bado hajahukumiwa anashikiliwa tu na police na mwendesha mashtaka anaangalia kama amfungulie mashtaka au la,so tafadhali rekebisheni hili ili msiipotoshe jamii.

    Kwa taarifa kamili ingia website ya bbc utapata hizo habari.

    Ahsante

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 27, 2016

    iwe funzo kwa wengine - Kupiga wanawake na kuwadhalilisha kuna madhara yake, unaweza ukavuna kile ulichopanda hapa hapa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...