Mama Theresa May (59) wa chamacha Wahafidhina (Conservative Party) leo ameteuliwa rasmi kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza wa pili mwanamke (baada ya Margaret Thatcher  aliyeongoza kati ya mwaka 1979 hadi 1990  na Waziri mkuu wa 12 tokea utawala wa Malkia Elizabeth, na Waziri Mkuu wa 76 wa Uingereza) katika hafla ya faragha iliyofanyika katika kasri ya Malkia Elizabeth jijini London. Na tayari Malkia amemwomba aunde serikali, kuirithi ya Waziri Mkuu wa zamani David Cameron aliyeachia ngazi baada ya kura ya maoni iliyowafanya Waingereza wajitoe Umoja wa nchi za Ulaya.
Waziri Mkuu wa zamani David Cameron aliyeachia ngazi baada ya kura ya maoni iliyowafanya Waingereza wajitoe Umoja wa nchi za Ulaya na familia yake wakiondoka 10 Downing Street ambayo ni ofisi na makazi rasmi ya Waziri Mkuu wa Uingereza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...