Meneja Ruzuku wa Vodacom Tanzania Foundation Sandra Oswald(wapili kushoto) akipatiwa maelekezo na Mariam Jecha (wapili kulia)ambaye ni bibi masoko wa kikundi cha 2 Seeds kilichopo kijiji cha Tabora Wilaya ya Korogwe Tanga , juu ya utengenezaji na upakiaji wa viazi na mihogo vinavyozalishwa na kikundi hicho baada ya kupata mafunzo ya ujasiliamali toka taasisi isiyo ya kiserikali ya 2Seeds ya nchini Marekani yenye makazi yake makuu Wilayani humo, Mradi huo inafadhiliwa na Vodacom Tanzania Foundation,wengine kwenye picha ni wajumbe wakikundi hicho.
Meneja Ruzuku wa Vodacom Tanzania Foundation,Sandra Oswald (kulia) akishirikiana na wanakikundi cha 2Seeds, wa kijiji cha Tabora Wilaya ya Korogwe Tanga kumenye viazi kwa ajili ya kutengenza Clips wakati alipotembelea kikundi hicho kukagua maendeleo ya miradi mbalimbali ya ujasiliamali ,ufugaji, Kilimo iliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania Foundation kwa kushirikiana na shirika lisilo la Kiserikali la 2Seeds Network la nchini Marekani na kufanya kazi zake nchini ambapo makazi yake makuu yapo Wilayani Korogwe.
Mwenyekiti wa kikundi cha 2Seeds kilichopo kijiji cha Tabora Korogwe Tanga,Asha Rajab akimuonyesha Meneja Ruzuku wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald ( kushoto) moja ya mifuko yenye embe iliyotengenezwa kitalaam, tayari kwa kupelekwa sokoni, kwa mauzo. Kikundi hicho ni miongoni mwa vikundi Vinne vilivyopata elimu ya ujasiriamali ,ufugaji,kilimo kwa ufadhili wa Vodacom Tanzania Foundation kwa ushirikiano na shirika lisilo la Kiserikali la 2Seeds Network la nchini Marekani na kufanya kazi zake nchini.
Mwenyekiti wa kikundi cha 2Seeds kilichopo kijiji cha Tabora Korogwe Tanga,Asha Rajab (Kulia)akimuonyesha Meneja Ruzuku wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald ( kushoto) moja ya mashine ya jua inayotumika kukaushia embe,na mbogamboga iliyotengenezwa kitalaam, wakati alipotembelea kikundi hicho kujionea maendeleo ya miradi mbalimbali ya ujasiriamali,Iliyofadhiliwa na Vodacom Tanzania Foundation kwa ushirikiano na shirika lisilo la Kiserikali la 2Seeds Network la nchini Marekani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...