Shirika la ndege la RwandAir limepokea ndege yake mpya aina ya Airbus A330 jana nchini Rwanda yenye uwezo wa kubeba abiria 276. Ndege hiyo mpya inakuwa ndege ya kwanza kufika Kigali ikiwa ni miongoni mwa ndege mpya nne zilizoagizwa. Mwisho mwa mwaka huu ndege hizo zitaanza kuruka kutokea mjini Kigali kuelekea nchi za India na China zikiwa ni safari mpya kwa Shirika hilo la RwandAir. Meneja mkazi wa Shirika hilo hapa nchini, Ibrahim Bukenya amesema mafanikio hayo ni kwa ushirikiano wa wasafiri na washiriki wao kwenye biashara.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...