Na Henry Mdimu
Mtangazaji machachari wa vipindi vya TV aliyevunja rekodi katika ukosoaji uliotukuka, Salama Jabir (pichani) ametajwa kuwa ndiye atakayeendesha tuzo za EATV Jumamosi ijayo  katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Roy Mbowe, Mratibu Mkuu wa tunzo hizo amable pia ni mkuu wa Masoko wa EATV amemtaja mwanadada huyo jana usiku saa nne kwamba ndiye atakayekuwa Mc kwa masaa matatu mfululizo akiongoza shughuli hiyo ambayo itarushwa live na kituo cha EATV pekee.
Jumla ya tuzo tisa zitatolewa kwa wasanii wa muziki na filamu waliofanya vyema kwenye tasnia hiyo huku tuzo moja ya heshima ikitolewa kwa mdau mwenye mchango uliotukuka katika tasnia ya sanaa kwa mwaka 2015/16.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...