Wateja wa Vodacom Tanzania wameletewa promosheni mpya inayojulikana kama”Nogesha Upendo”ambayo itawawezesha wateja wake kujishindia zawadi ya fedha taslimu ,muda wa bure wa maongezi na MB za Interneti kila siku katika msimu huu wa sikukuu. Zawadi zenye thamani ya shilingi Bilioni 5 zitatolewa kwa wateja ambapo wateja wapatao 500 wataweza kujishindia shilingi milioni 1kila mmoja katika kipindi chote cha msimu wa promosheni.

Akiongea wakati wa uzinduzi ,Afisa Mtendaji Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia alisema “Vodacom Tanzania tunayo furaja kuzindua promosheni ya msimu wa sikukuu ya Nogesha Upendo inayolenga kuleta shamrashamra za furaha ya sikukuu kwa wateja wetu.

Tunajua sikukuu hizi zinaleta familia za kitanzania na marafiki pamoja kufurahi na kutumiana salamu za upendo, tumeleta promosheni hii kwa ajili ya kuwazadia wateja wetu wote kila wanaponunua vifurushi vya muda wa maongezi na Data kila siku. ”Promosheni hii itawezesha wateja wetu 500 kujishindia kila mmoja shilingi milioni 1/- katika droo za wiki na wengine watajishindia shilingi 100,000/- katika droo za kila siku katika msimu huu wa sikukuu kupitia promosheni hii”.

Aliongeza kusema “Mbali na wateja kujishindia dakika tano za muda wa bure wa maongezi na kuperuzi internet,wateja wa Vodacom pia kila watakaponunua vifurushi wataingizwa kwenye droo za kila siku na kila wiki za kujishindia vitita vya fedha.Kiasi cha shilingi milioni 700 zimetengwa kwa ajili ya kuwazawadia wateja wetu katika msimu huu wote wa sikuu”.

Kwa ujumla, Vodacom imetenga zawadi zenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 5/- kwa ajili ya kuzawadia wateja wake kwa njia ya fedha taslimu, muda wa maongezi na bando za intaneti(MB). Promosheni hii itakayodumu kipindi cha miezi 2 kuanzia leo ni kwa ajili ya wateja wote wa Vodacom ambao laini zao ziko hewani na watakanunua vifurushi vya kupata huduma mbalimbali za kampuni.

“Promosheni ya Nogesha Upendo imebuniwa kwa ajili ya kuwashukuru wateja wetu kwa kutuunga mkono muda wote, Tunawatakia heri katika msimu wa sikukuu na tunawakumbusha wakati wote kufuatilia zawadi watakazokuwa wanazishindia kutoka mtandao wa Vodacom kuanzia muda wa maongezi na fedha taslimu zitakazowawezesha kufurahia sikukuu pamoja na familia zao na marafiki. Hivi ndivyo Vodacom tumejizatiti kufanya Maisha ya wateja wetu kuwa murua na kusambaza upendo”alisisitiza Mworia.
  Afisa Mkuu wa Masoko wa Vodacom Tanzania,Ashutosh Tiwary (kushoto)na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, Nandi Mwiyombella (kulia) wakimsikiliza Afisa Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Uhusiano wa Kampuni hiyo, Rosalynn Mworia (katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Promosheni ya”Nogesha Upendo” leo jijini Dar es Salaam itakayowawesha wateja wa kampuni hiyo kujishindia muda wa maongezi,Vifurushi vya intaneti pamoja na  fedha taslimu, shilingi Bilioni 5/- zimetengwa kwa ajili ya promosheni hii ambapo wateja 500 watajishindia shilingi Milioni 1/- kila mmoja  kupitia droo za kila wiki kwa msimu huu wa sikukuu.

Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kuzinduliwa rasmi Promosheni ya Nogesha Upendo leo jijini Dar es Salaam itakayowawesha wateja wa kampuni hiyo kujishindia muda wa maongezi,Vifurushi vya intaneti pamoja na  fedha taslimu, shilingi Bilioni 5/- zimetengwa kwa ajili ya promosheni hii ambapo wateja 500 watajishindia shilingi Milioni 1/- kila mmoja kupitia droo za kila wiki kwa msimu huu wa sikukuu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...