Na Anthony Ishengoma-MCDGC.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inakusudia kuanzisha Dawati la Ulinzi la na Usalama katika shule zote  pamoja na Kamati za Ulinzi na Usalama katika ngazi ya Kata na Vijiji Nchini kote ili kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Sihaba Nkinga amesema hayo wakati akiongea katika ufunguzi wa Kikao cha Kamati Kuu cha Baraza la Watoto la Taifa kinachofanyika kwa siku mbili Mjini Morogoro.

Aidha amewataka wajumbe wa Kikao hicho kujadiliana kwa kina juu ya ongezeko la vitendo vya ulawiti na ubakaji dhidi ya watoto na kuwasilisha mapendekezo yao Wizarani  akisema kuwa hivi karibuni vitendo hivyo vimeongezeka kwa wingi sana katika Jamii.

Aliongeza kuwa kufuatia kuzinduliwa kwa Mpango Mkakati wa Kupambana na Kuzuia Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto wa miaka mitano Serikali itahakikisha vitendo vya ukatili vinapunguzwa kwa asilimia hamsini kupitia mpango kazi huo na kuongeza kuwa vitendo vya ukatili kwasasa vinatofautiana viwango akitaja ukatili huo kuwa ni ubakaji, ulawiti, ukeketeji, mimba na ndoa za utotoni.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Taifa  Caroline Augustino akiongea na vyombo vya Habari baada ya ufunguzi huo kuwa pamoja na kukutana leo jijini Morogoro pia Baraza hilo limefanya ziara mbalimbali mikoani kwa lengo la kuandaa makala maalumu za uelimishaji jamii kwa njia ya radio na runinga ili jamii iweze kufahamu maana  na aina za ukatili dhidi ya watoto.
 Mwenyekiti wa Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ameir Haji Khamis akiongea na wajumbe wa baraza hilo katika kikao cha kamati kuu cha tatu cha Baraza la watoto la taifa leo Mjini Morogoro,Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga na Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo Caroline Augustino.
 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Watoto kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi.Margareth Mussai akiongea na watoto kutoka Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa kikao cha kamati kuu cha tatu cha Baraza la watoto la taifa na kuwapongeza kwa kazi wanazoendelea kuzifanya kwa maslahi ya watoto nchini Leo Mjini Morogoro, Kulia ni Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga akiongea na watoto kutoka Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa kikao cha kamati kuu cha tatu cha Baraza la watoto la taifa ambapo aliwataka katika agenda zao wajadili ukatili dhidi ya ubakaji na ushoga na hatimaye wampelekee taarifa ili kujua nini serikali ikifanye, Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ameir Haji Khamis na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Watoto Bi.Margareth Mussai 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...