Kama inavyojulikana kuwa Mrembo wa Miss Universe Tanzania 2016 Jihan Dimack aliyetwaa taji la Miss Universe Tanzania mapema mwezi wa kumi na moja mwaka 2016 aliondoka nchini tangu tarehe 11 Januari kuelekea Manilla nchini Philipines kwa ajili ya kushiriki Mashindano ya Miss Universe kwa ngazi ya kimataifa .

Jihan Dimack akiungana na wenzake kutoka nchi mbalimbali Ulimwenguni yupo nchini Phillipines kwa muda wa wiki mbili sasa akiiwakilisha vyema Tanzania katika kuwania taji hilo.

Mashindano haya ambayo yanazingatia vigezo mbalimbali pia yana utaratibu wa upigaji kura ambao umeshaziduliwa rasmi tangu tarehe 23 Januari 2017 na kura zitapigwa ndani ya siku sita hadi tarehe 30 Januari 2017 ambayo ndo finali za mashindano hayo.

Utaratibu uliowekwa na uongozi wa Miss Universe mwaka huu ni kwamba kutakua na warembo 12 bora na kati ya hao kumi na mbili mrembo mmoja ataingia kwa kigezo cha kupata kura nyingi kupitia mtandoni.

Hivyo basi Watanzania wote kwa pamoja tushirikiane katika hili kuhakikisha mrembo wetu kutoka Tanzania Jihan Dimack anapata kura za kutosha kumuwezesha kuingia katika fainali hizo.

Itakua jambo la faraja sana kufanikisha ushindi kwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa kupiga kura kwa wingi na kila mtu mmoja ana uwezo wa kupiga mpaka kura kumi kwa siku. Ushindi wa mrembo wetu upo mikononi mwetu wenyewe.

Ili uweze kumpigia kura mrembo wetu Jihan utatakiwa kufanya mambo machache yafuatayo:

Jinsi ya kumpigia kura Jihan katika mashindano ya Miss Universe kuanzia tarehe 23 January 2017:
1) VODI: Pakua Vodi app katika Google Store au Apple Store
2) Kupitia tovuti ya www.missuniverse.com
3) MISS U APP: Pakua Miss U app 
4) TWITTER: Tweet kwa kutumia hashtag #MissUniverse alafu utatumia hashtag maalum ya Jihan itakayotolewa muda si mrefu. 

Tafadhali kumbuka kwa kila mtu ataweza kupiga kura mara 10 kwa siku kwa kila akaunti aliyoisajili.
***Kumbuka kuwa website ya missuniverse.com ni mtandao pekee ambapo upigaji kura utaendeshwa.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...