Na Raymond Mushumbusi WHUSM.

Serikali imeahidi kuendelea kushirikiana na vyombo vya habari nchini katika kutoa habari kwa ajili ya kuhabarisha umma kuhusiana na mambo mbalimbali yahusuyo Serikali katika kutekeleza majukumu yake.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipotembelea na kujionea utendaji kazi wa Kampuni ya IPP Media kwenye vituo vya Televisheni vya ITV, EATV na Capital Tv pamoja na Sahara Media kwa tawi la Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo Mhe. Nape Moses Nnauye amehaidi kuendeleza ushirikiano baina ya Serikali na vyombo vya habari katika utoaji wa habari ambazo ni muhimu kwa wananchi kujua zikiwemo hatua ambalimbali zinazochukuliwa na Serikali katika kutekeleza majukumu yake katika kuwaletea wananchi maendeleo.

“Niseme kwa kipindi cha nyuma kumekuwa na urasimu wa utoaji wa taarifa muhimu kutoka kwetu kuja kwenu vyombo vya habari lakini niwahakikishe kuwa sasa Serikali imefungua milango kwenu na tuendelee kushirikiana katika kuhabarisha umma wa watanzania” Alisistizia Mhe. Nnauye.

Kawa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abass amevihakikishia vyombo vya habari nchini ushirikiano mzuri katika kupata habari za Serikali kutoka katika vitengo vyote vya Mawasiliano Serikalini.

Dkt Abass ameeleza kuwa kwa sasa wako katika mpango wa kuboresha vitengo vya Mawasiliano serikali ili kuboresha upatikanaji wa habari zinazohusu Serikali.

“Niwahakikishieni ndugu zangu wanahabari kuwa suala la upatikanaji wa habari kutoka Serikali litakuwa si la kusumbuana tena na tunatengeneza mfumo katika vitengo vyote vya Mawasilaino Serikalini ili iwe rahisi kupata taarifa kutoka kwetu” alisisitiza Dkt Abass.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na uongozi na  baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya IPP Media yenye vituo vya Televisheni vya ITV, EATV na Capital Tv alipotembelea na kujionea utendaji kazi wa vituo hivyo Leo January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abass(kushoto) akifafanua jambo kwa uongozi na wafanyakazi wa IPP Media upande wa Televisheni wakati Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye  alipotembelea Kampuni ya IPP Media kwenye vituo vya Televisheni vya ITV, EATV na Capital Tv Leo January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza mara baada ya kuwasili katika kampuni ya IPP media kwa ajili ziara yake ya kujionea utendaji kazi wa vituo vilivyo chini ya Kampuni hiyo Leo January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiangalia studio ya kutangazia habari katika kituo cha Televisheni cha ITV alipofanya ziara kujionea utendaji kazi wa vituo vilivyo chini ya IPP Media Leo January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Sahara Media kwa upande wa Dar es Salaam Bw. Cyprian Musiba akifafanua jambo kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipotembelea Sahara Media kwa upande wa Dar es Salaam kujionea utendaji wake wa kazi Leo January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...