Upatikanaji wake ni rahisi, wa haraka
na ni huduma
salama ya kibenki kupitia mtandao
Benki ya Stanbic
Tanzania imezindua huduma mpya ya malipo kupitia intaneti na simu za mkononi
inayoambatana na huduma nyinginezo zinazolenga kuboresha ukusanyaji wa pesa na
ufanyaji wa malipo kwa mashirika na biashara mbali mbali, ikiwa ni sehemu ya
jitihada zake za kutoa huduma rahisi na salama za kibenki
Akizungumza
katika uzinduzi wa huduma hiyo jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo cha
Bidhaa na Huduma za Miamala wa Benki hiyo, Bw. Charles Mhina alisema mabadiliko
hayo ya ufanyaji malipo na makusanyo yaani malipo ya pamoja kupitia internet na
mitandao na uwekaji fedha benki – yatawahakikishia wateja wa benki katika sekta
mbalimbali maboresho makubwa katika utoaji huduma
Akizindua huduma
hiyo ya kipekee katika soko ijulikanayo kama Malipo ya Pamoja Kupitia simu (
Mobile Bulk Payment), Bw. Mhina alisema huduma hiyo itayawezesha mashirika
kufanya malipo kutoka katika akaunti zao za Stanbic kwenda kwenye mitandao
mbali mbali ya simu ikiwa ni pamoja na Tigo Pesa, Airtel Money,Mpesa na Ezypesa
wakati wowote na popote walipo
Alisema Malipo
ya Pamoja kupitia Simu yatatolewa kupitia mfumo wa utoaji huduma mtandaoni wa
benki hiyo, ambao unawahakikishia wateja upatikanaji wa huduma wakati wowote, kwa
njia rahisi, ya haraka na salama, jambo linaloongeza ufanisi zaidi katika ufanyaji
wa miamala yao ya kibiashara.
“Uzinduzi wa
huduma hii ni uthibitisho wa jitihada za Benki ya Stanbic katika kuboresha
huduma zetu za ufanyaji miamala, lengo kuu likiwa ni kuleta tija katika
biashara za wateja wetu,” alisema Bw. Mhina
Akizungumzia juu
ya huduma ya malipo bila kutumia pesa taslim (Till to Bank Cashless Payment) ambayo
itawawezesha wafanyabiashara kupokea malipo ya moja kwa moja kutoka katika
mitandao ya simu, Bw. Mhina alisema huduma hiyo itaruhusu wamiliki wa akaunti
za biashara kupokea malipo kupitia Mpesa, Tigopesa na Airtel Money kutoka kwa
wateja wao kupitia namba maalum na fedha zitaelekezwa moja kwa moja kwenye
akaunti zao za Benki za Stanbic
Alieleza kwamba
kutokana na kuwa soko limetawaliwa na pesa taslim, huduma hii imelenga katika
kupunguza mzigo mkubwa kwa wafanyabiashara wa upokeaji wa malipo ya fedha
taslim na kubadilisha tabia ya wateja kwenda kwenye malipo ya mtandao
“Benki ya
Stanbic ipo katika mstari wa mbele katika ugunduzi. Leo hii pia tunatambulisha
huduma ya Till-to-Bank kwa wateja wetu. Malipo kupitia mtandao sasa yameyapita
malipo ya pesa taslim na tunatizamia kuwa asilimia kubwa ya malipo hayatakuwa
ya fedha taslim katika miaka michache ijayo. Tumesimama katika mhimili wa
kulirahisisha hili kwa wateja wetu,” alisema.
Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa na Huduma za Miamala wa Benki ya Stanbic
Tanzania, Bw. Charles Mhina(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari
wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya malipo kupitia internet na simu za
mkononi inayoambatana na huduma nyinginezo zinazolenga kuboresha
ukusanyaji wa pesa na ufanyaji wa malipo kwa mashirika na biashara mbali
mbali jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni mkuu wa kitengo cha
upatikanaji wa huduma kwa wateja wa benki hiyo, Allen Chiombola.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...