Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Angellah Kairuki amesema kwamba
serikali itahakikisha kwamba Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) tawi la Mbeya
kinakuwa na majengo yake ili kupunguza gharama za uendeshaji.
Kwa sasa chuo hicho kinatumia majengo ya
kukodi ambayo ni mali ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya,majengo hayo yapo eneo la
soko Matola, Chuo kinahudumia wakazi wa
Nyanda za Juu Kusini.
Akiwasilisha taarifa ya Chuo cha Utumishi wa
Umma Tanzania tawi la Mbeya mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala na
Serikali za Mitaa Waziri Kairuki alisema gharama ya kodi ya shilingi
milioni 24 kwa mwezi ni kubwa na kwamba serikali iko katika mchakato wa
kuhakikisha kwamba chuo hicho kinamilikishwa mjengo hayo ili kupunguza gharama
za uendeshaji.
Aidha Waziri
huyo alisema kwamba serikali itahakikisha kwamba chuo kinakuwa na wakufunzi wa
kutosha ili kuendesha kozi zake kwa ufanisi.
Mkuu wa TPSC Dk.Henry Mambo aliiambia kamati
hiyo kuwa tawi la Mbeya linakua kwa kasi kwani kwa sasa lina wanafunzi 1236,
tawi hilo lilizinduliwa mwaka 2014 likiwa na wanafunzi 453.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge
Utawala na Serikali za Mitaa Mhe. Jason Rweikiza akizugumza na watumishi wa Chuo cha
Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) tawi la Mbeya pamoja na wajumbe wa kamati hiyo
hawapo pichani katika Ukumbi wa chuo hicho Jijini Mbeya, kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Angellah
Kairuki,
kulia ni Mkuu wa TPSC Dk.Henry Mambo. Picha na Kenneth Ngelesi
Mkurugenzi
wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Tawi la Mbeya Dk. Heriel Nguvava
katikati akiwaonyesha chumba cha Kompyuta wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge
Utawala na Serikali za Mitaa walipofanya ziara chuo hapo kushoto ni Mwenyekiti wa kamati
hiyo Mhe. Jason Rweikiza kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki. Picha na Kenneth Ngelesi. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...