Tunapenda
kutaarifu Umma kuwa kuna mtu aliyefungua ukurasa katika mtandao wa kijamii wa ‘Twitter’
kwa kutumia jina la Mhe. Charles Mwijage
(MB), Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji na kuweka taarifa kuwa “Kilichotokea
kwa Clouds Media ni kitendo cha kinyama na wala si uungwana kabisa tunajenga
nchi ya viwanda na si ya kutishana”
Wizara
inakanusha taarifa hiyo ya kizushi iliyosambaa katika mitandao mbalimbali ya
kijamii yenye lengo la kuleta chuki na kuchafua jina la Waziri pamoja na Wizara
yetu kwa ujumla.
Wizara
inachukua hatua za kisheria kuwatambua wale wote waliohusika na kutengeneza
ukurasa huo bandia.
Tunatoa
wito kwa wahusika wote kuacha mara moja kusambaza taarifa hii potofu.
IMETOLEWA NA
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI,
WIZARA YA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI
22 March, 2017
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...