Kamishna Jenerali wa
Uhamiaji Dr. Anna Peter Makakala ,akimvisha cheo kipya Kamishna wa Uhamiaji
Utawala na Fedha, Edward Peter Chogero katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi
wa Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma. Anayeshuhudia ni
Naibu Kamishna wa Uhamiaji Chrispin Ngonyani. Tukio hili linehudhuriwa na
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest
Rwegasira na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Hassan Simba Yahaya.
Kamishna mpya wa Uhamiaji
Divisheni ya Sheria Hannerole Morgan Manyanga akila kiapo cha Utii mbele ya Kamishna
Jenerali wa Uhamiaji Dr. Anna Peter Makakala
katika hafla iliyofanyika leo katika
ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma. Hafla hiyo imehudhuriwa
na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira
na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo Balozi Hassan Simba Yahaya.
Kamishna wa Tume ya Maadili
ya Utumishi wa Umma , Jaji Mstaafu Harold Nsekela wa kwanza kushoto akiwaongoza
Makamishna wapya wa Uhamiaji kuapa kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Utumishi wa Umma baada ya Makamishna hao wapya
kuvalishwa vyeo vipya katika hafla
iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mikutano
wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.
Makamishna wapya wa Uhamiaji
wakisaini Fomu za Maadili ya Viongozi wa Umma baada ya Makamishna hao kula
kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Utumishi wa Umma, katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi
ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali
Projest Rwegasira akizungumza jambo na Makamishna wapya wa Uhamiaji
baada ya kumalizika shughuli ya kuapishwa Makamishna hao leo katika viwanja vya Ofisi ya Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...