Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack ameagiza wakurugenzi wa mamlaka za Serikali za Mitaa na Maji kuhakikisha hakuna mtu anayefanya shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo vya maji.

Telack alitoa agizo hilo juzi wilayani hapa katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese wakati wa kilele cha maadhimisho Wiki ya Maji yaliyofanyika kijiji cha Sekeididi.

Aliagiza wakurugenzi hao kuhakikisha vyanzo hivyo vinapandwa miti ili kutunza uoto wa asili ambao mara nyingi huathiriwa na ukame kutokana na kukosekana kwa miti.Mkuu huyo wa mkoa aliwataka viongozi hao wasimamie utekelezaji wa sheria ya utunzaji wa mazingira ili kunusuru vyanzo vya maji, kwani Serikali inatumia fedha nyingi katika utekelezaji wa miradi ya maji.

“Utunzaji wa vyazo vya maji ni jambo muhimu katika upatikanaji wa maji na hivyo ni jukumu la kila mmoja wetu kutunza vyanzo vya maji kwa kupanda miti eneo linalozunguka vyanzo.“Kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004, kifungu cha 57, kifungu kidogo cha 1 kinakataza mtu yeyote kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya mita 60 kwenye vyanzo vya maji,” alisema.

Maadhimisho hayo yaliambatana na zoezi la upandaji miti kwenye bwawa la Sekeididi ambalo litakuwa likitoa huduma ya maji kwa wananchi wa maeneo hayo.Telack aliwataka wananachi kuiunga mkono Serikali katika jitihada zake za kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo yao.
Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese akisoma hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Maji kimkoa
Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese akipanda mti wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Maji kimkoa.
Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese (katikati) akiongozwa na Kaimu Mhandisi wa Maji, Wilaya, Bernad Bwire (wa pili kushoto) kutembelea bwawa la maji na kupanda miti katika kilele cha Wiki ya Maji. Wengine pichani kushoto ni mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mohamed Mlewa (kushoto) na Kaimu Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari, Steven Cleophace (kulia).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...