NA BALTAZAR MASHAKA,MISUNGWI

KERO ya uhaba wa maji iliyokuwa ikiwakabili wananchi zaidi ya 1000 wa vitongoji vitano vya Kijiji cha Kasololo wilayani Misungwi mkoani Mwanza na kusababisha ndoa nyingi kuvunjika pamoja na migogoro kwenye familia, imetatuliwa baada ya Taasisi ya The Desk & Chair Foundation kuchimba na kujenga visima saba.

Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation tawi la Tanzania Sibtain Meghjee akikabidhi visima hivyo vilivyogharimu sh 21 milioni alisema walisitisha ujenzi wa Msikiti (nyumba ya ibada ) ili watatue kero ya maji kwa kuwapa wananchi huduma ya maji itakayowanufaisha watu zaidi ya 1200 kwa matumizi ya kibinadamu.

Alisema visima vimekabidhiwa ili kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Bi. Fatma AS. mjukuu wa Mtume Mohamed S.A.W.ambaye alifanya kazi kubwa ya kusaidia jamii lakini pia miradi ya kijamii inayofadhiliwa na waumini wa madhahebu ya Shia Ithna Asheri, kwenye maadhimisho hayo ilikabidhiwa huko Kwimba Mwanza na Kondoa mkoani Dodoma na maeneo mengine nchini.
Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation tawi la Tanzania Sibtain Meghjee akimtwisha ndoo ya maji milembe Kuhamwa, Mwenyekiti wa Kiyongoji cha Mwashileko katika Kijiji cha Kasololo wilayani Misungwi Mwanza, ikiwa ni ishara ya kukabidhi kisima cha maji safi na salama kati ya saba vilivyochimbwa na taasisi hiyo kwa gharama ya sh. 21 milioni.
Mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Kasololo katani humo katika Wilaya ya Misungwi aichota maji baada ya kukabidhiwa kisima cha maji kilichochimbwa na taasisi ya The Desk & Chair Foundation ili kuwapunguzia ya kero ya maji inayowakabili kwa muda mrefu.
Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation Sibatain Meghjee (kushoto nyuma ya pump ya maji) akizungumza na wananchi baadhi wa Kijiji cha Kasololo katika Wilaya ya Misungwi baada ya kuwakabidhi moja ya visima vilivyochimbwa na taasisi hiyo hivi karibuni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...