Bujumbura,Burundi

Nchi wanachama wa Umoja wa Afika mashariki pamoja na sektarieti ya umoja huo(EAC) wamehimizwa kuharakisha mchakato wa kuhakikisha kada zingine za afya ikiwemo ya uuguzi na kada nyingine zenye sifa na viwango vinavyofanana na madaktari kuajiriwa kwenye nchi yeyote ya Afrika Mashariki

Hayo yamesemwa jana na Waziri WA Afya,Maedeleo ya Jamiii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Kisekta la mawaziri wa Afya wa Afrika mashariki kwenye kikao cha 14 nchini hapa

Waziri ummy alisema amefurahishwa sana na hatua iliyofikiwa na nchi wanachama wa Jumuiaya hiyo ambapo hivi sasas madaktari wanaotoka katika jumuiya hiyo kuajiriwa

Katika hatua nyingine kikao hivho kimejadili kuhusu kuimarishwa kwa mafunzo na usimamizi wa pamoja wa waraalam wa afya,udhibiti wa magonjwa ya milipuko pamoja na magonjwa ya kuambukiza kama vile Ebola,Mafua makali ya ndege kifua kikuu(TB) na UKIMWI 
Picha ya pamoja ya mawaziri wa jumuiya ya umoja wa Afrika Mashariki Mara baada ya ufunguzi wa Kongamano LA kupanga jinsi ya kukabiliana na majanga.Kongamano hilo lilizinduliwa na Rais Pierre Nkurunzinza Mganga Mkuu wa Serikali toka Tanzania (wa kwanza kushoto) Prof.Bakari Kambi akichangia mada katika mkutano huo uliokutanisha wadau wa afya kutoka Afrika mashariki.  Baadhi ya wajumbe toka Kenya wakifuatilia mada zilizowasilisha kwenye mkutano huo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...