Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Nyabaganga Taraba amewaagiza maofisa ugani wa kata zote kuhakikisha wanawafikia wakulima na kuwafundisha mbinu bora za kilimo chenye tija.

Ameagiza pia wananchi kulima mazao yanayostahimili ukame hususan mtama na uwele badala ya kuwa na kasumba ya kung’ang’ania kilimo cha mahindi ambacho katika sehemu kubwa ya wilaya hakifanyi vizuri.

Taraba alitoa agizo hilo wakati wa ziara yake kwenye mashamba ya mtama katika kata za Uchunga, Mwaweja na Ukenyenge kujionea na kufanya tathmini ya kilimo wilayani humo.

Aliwataka maofisa hao kujiwekea utamaduni wa kutembelea mashamba ili kuwafundisha namna ya matumizi ya mbegu bora kwani wengi wao hupanda bila utaalamu.

Aliwataka kusimamia Sheria ndogo ya mwaka 2008 ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu inasisitiza kuwa kila kaya wilayani humo iweze kulima ekari mbili za mazao yanayostahili ukame ambayo ni mtama.

Mkuu wa wilaya hiyo alisema kuwa hata hivyo wakulima wengi wilayani humo wameweza kutekeleza sheria ndogo hiyo lakini wamepata changamoto mbalimbali zikiwemo ukosefu wa maarifa ya matumizi ya aina sahihi za mbegu.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba akionesha masuke ya zao la mtama wakati akikagua mojawapo ya mashamba ya wakulima wa Kata ya Mwaweja wakati wa ziara yake.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba (wa pili kulia) akibadilishana mawazo na mkulima, Sendama Luhende, Ofisa Kilimo, Sarai Pura na mkulima Mariam Nkinga wakati wakikagua shamba.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu akiendelea kukagua shamba la mtama katika Kata ya Mwaweja..

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...