Wakazi wa Nchi ya Falme za Kiarabu na wasafiri wa kimataifa watajionea maeneo mbalimbali ya vivutio vinavyopatikana Abu Dhabi kwa siku mbili tu. Shirika la Ndege limezindua shindano hilo kwenye Instagram na zawadi zaidi ya 500 zitashindaniwa.

Shirika la Ndege la Etihad limeamua kuwazawadia mamilioni ya wageni wanaosafiri kupitia makao makuu pamoja na wakazi wa nchi ya Falme za Kiarabu kwa kuleta shindano linalofanyika angalau mara moja kwa mwaka na kuwahusisha watu wote kwa siku mbili.

Kampeni hiyo ya 48 Hour Challenge ni sehemu ya shughuli za Etihad katika kupanua wigo wa kuitangaza Abu Dhabi kama sehemu nzuri ya mapumziko kwa wasafiri na watu wanaopenda kuishi katika nchi ya Falme za Kiarabu hasa wanaopenda kutembelea wakati wa likizo fupi. Wakiwa kwenye jiji hilo watapata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ambayo yameandaliwa kupitia programu hiyo.

Kampeni hiyo ya Shirika la Ndege la Etihad itazinduliwa na msanii maarufu kutoka Uingereza anayetambulika kwa jina la Rick Wilson ambaye atatangaza jinsi watu wanavyoweza kunufaika na ofa hiyo ya saa 48 wakiwa Abu Dhabi.

Baadhi ya video zake zitaonyesha ofa katika maeneo ya vivutio vya Abu Dhabi. Pia, video za kampeni hiyo zitaonekana kupitia mtandao ambapo wateja watashare na wenzao katika mitandao ya kijamii. Pia wataweza kuona kupitia chaneli za kwenye ndege wanaposafiri.

Wilson alisema, “Kwangu mimi nilijua hii inaamanisha kukaa uwanja wa ndege, au kusafiri bure lakini sivyo kampeni hiyo inavyomaanisha.” 

“Mtu atapata fursa ya kusafiri katika ukanda wa jangwa ikiwa ni pamoja na kutembela maeneo ya kuvutia ya kiutamaduni. Abu Dhabi imenifunza kuwa kutembelea maeneo mbalimbali nikiwa safarini ni sehemu mojawapo ya kuburudika. Hii inaweza kuwa ni miongoni mwa njia nzuri za kupumzika na kujiweka katika hali ya kujisikia vyema. Vilevile nimepata muda wa kujionea mambo mengi kwenye nchi hii. Niwapo safarini sitarudia tena kukaa tu uwanjani na kusubiri ndege tu.”

“Abu Dhabi ni sehemu nzuri, yenye joto kiasi na watu wake wenye ukaribu wa hali ya juu. Mji huu una kila kitu kinachohusiana na mapumziko. Kuna sehemu tulivu na maeneo mazuri ya kutembelea. Ni mji unaovutia na kupendeza ambao una vitu vya kipekee unavyoweza kujionea kwa muda mfupi na kwa wakati.”

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Etihad, Peter Baumgartner alisema, “Kuzinduliwa kwa programu hii ya Shirika la Ndege la Etihad kutawawezesha watu kutembelea maeneo mbalimbali wakati wakisubiri kusafiri.
Mohammad Al Bulooki, Makamu wa Rais Mtendaji wa Kitengo cha biashara cha Shirika la ndege la Etihad; Mhe. Saif Saeed Ghobash, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Utalii na Utamaduni (TCA) Abu Dhabi, Peter Baumgartner, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la ndege la Etihad wakisheherekea uzinduzi wa ndege shindano la masaa 48 la kuitangaza Abu Dhabi katika Soko la usafiri la Uarabuni.
Msanii maarufu kutoka Uingereza anayetambulika kwa jina la Rick Wilson akiruka matuta ya jangwa la Abudhabi wakati aliposhiriki shindano lililozinduliwa na Etihad la masaa 48 ili kuitangaza Abudhabi kwa wasafiri wake.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...