Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Sophia Mjema amewaomba wananchi hasa wa wilaya ya Ilala kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 29 mwezi huu katika kuukaribisha na kupokea Mwenge wa uhuru unaotaraji kukesha eneo la Kariakoo .

Mjema ameyasema hayo leo wakati akitembelea miradi mbali mbali inayoendelea na ujenzi katika manispaa ya Ilala kwa kuanzia eneo la Kivukoni ambapo mwenge utupokelewa na kuelekea sanamu ya askari uliopo katikati ya jiji, bustani ya Kaburi moja, na miradi mingineyo.

Amesema mwenge huo mwaka huu una kauli mbiu isemayo,’ mwenge ni kushiriki katika uchumi wa Viwanda’ na mwenge huu utakuwa unaongelea viwanda zaidi katika ukuzaji wa viwanda na ili kufanikisha hilo tutaenda maeneo ya gerezani ambapo kuna viwanda vidogo vidogo ambavyo tutavisaidia kukuza uchumi.

“Tunaomba wananchi washiriki zaidi katika kuukaribisha mwenge na katika mkesha ambao utakuwa pale kariakoo, tunapeleka mkesha kariakoo kwa sababu pale tunajaribu na tunataka kuwatambua wamachinga rasmi, tunataka kuwafugulia ofisi yao rasmi ili wawe wanatambulika na serikali”.

Ameongeza kuwa ili kukuza uchumi wa viwanda serikali itamsaidia kila mwananchi mwenye kiwanda kidogo katika kukuza uchumi wake ili baadae nao waweze kuja kuwa wajasiliamali wakubwa na hata kumaliza kabisa biashara ya wamachinga kama siyo kupunguza,.

Aidha amesema Wilaya ya Ilala itatenga mitaa kama vile, Kongo, Mchikichi, Sikukuu na Nyamwezi kutumika zaidi kwa shughuli za umachinga na mingine itakuwa kwa ajiri ya maegesho ya magari ya mizigo, Tax na huduma zingine kama hizo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akijadili jambo na Katibu tawala wa Wilaya hiyo Edward Mpogolo .
Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema akizungumza na afisa Mazingira wa Ilala , Abdon Mapunda juu ya umuhimu bustani hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema akipata Maelekezo ya bustani ya Kaburi moja kutoka kwa Mhandisi Faizer Mbange.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema, akikagu sehemu itakayopandwa miti na majani kwa ajili ya watu kupumzika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...