Kipa Aishi Manula, akichupa kudaka mpira wakati
wa mazoezi yanayosimamiwa na Kocha wa Makipa wa Taifa Stars, Patrick Mwangata
aliyepiga magoti katika mazoezi yanayofanyika
Kituo cha michezo cha Tolip (Tolip Sports City) hapa Alexandria, Misri. Taifa
Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti inayozalishwa na Kampuni ya Bia ya
SBL, inajiandaa kucheza na
Lesotho Juni 10, 2017 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania kucheza fainali za
Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon.
Kipa Said Mohammed
Nduda , akichupa kuzuia mpira wakati wa mazoezi yanayosimamiwa na Kocha wa
Makipa wa Taifa Stars, Patrick Mwangata aliyepiga magoti katika mazoezi yanayofanyika Kituo cha michezo cha Tolip
(Tolip Sports City) hapa Alexandria, Misri.
Kipa Benno Kakolanya,
akidaka mpira wakati wa mazoezi yanayosimamiwa na Kocha wa Makipa wa Taifa
Stars, Patrick Mwangata aliyepiga magoti katika mazoezi yanayofanyika Kituo cha michezo cha Tolip (Tolip Sports City)
hapa Alexandria, Misri.
Kiungo wa pembeni wa
Taifa Stars, Simon Msuva akiwa kwenye kasi kuwahi mpira wakati wa mazoezi ya
timu hiyo yanayofanyika Kituo
cha michezo cha Tolip (Tolip Sports City) hapa Alexandria, Misri.
Libero wa Taifa
Stars, Erasto Nyoni (katikati) akijitahidi kudhibiti mpira mbele ya
washambuliaji wenye njaa ya kufunga, Ibrahim Ajib (kulia) na Abderheman Mussa
kabla ya kipa Said Mohammed hajatokea kusaidia wakati
wa mazoezi ya timu hiyo yanayofanyika Kituo
cha michezo cha Tolip (Tolip Sports City) hapa Alexandria, Misri. Picha
na Alfred Lucas wa TFF.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...