BAADA ya baadhi ya vyombo vya habari kutangaza kuwepo mgogoro kati ya
wananchi na serikali katika Pori tengefu la Mkungunero wilayani Kondoa
mkoa wa Dodoma, mkuu wa wilaya hiyo amejitokeza na kudai taarifa hizo
hazina ukweli.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mkuu wa Wilaya
ya Kondoa Bibi Sezaria Makota, alisema habari zilizosambazwa kuhusiana
na wananchi kunyanyaswa katika pori la Mkungunero zinazungumzia
matukio ya zamani ambayo kimsingi yameshapatiwa ufumbuzi na serikali.
“Katika taarifa zilizotolewa kwenye vyombvo vya habari imeelezwa kuwa
viongozi na wanakijiji katika Kijiji cha Kisondoko na Kata ya KK kuwa
wananyanyaswa na kuna wasichana walisema wamebakwa lakini nakanusha
taarifa hizi si za kweli, wafanyakazi wa pori la Mkongonero
wanajiheshimu na wanafanya kazi kwa nidhamu,” alisema Bi. Makota na
kuongeza:
“Nilipofika Kondoa mwaka jana (2016) nilisikia hayo malalamiko lakini
nilipofuatilia nikabaini si kweli, viongozi wa kamati ya ulinzi na
usalama waliitisha mkutano kuwahoji wanakijiji wanaosema
walinyanyashwa, kupigwa na kubakwa, kulikuwepo na madaktari
waliowafanyia vipimo lakini hakuna aliyeonekana amebakwa.”
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...