MWAZILISHI na mchungaji Mkuu wa kanisa  la Moto halisi (Pure Fire miracles Ministries International'), lililopo Tabata Segerea kwa Bibi
,Dk. Enoch Aminu kutoka nchini Ghana amewasili hapa kwaajili ya
  kuwaletea siku tatu za huduma ya ujazo wa upako.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumkaribisha hapa nchini mchungaji huyo kutoka nchini Ghana, Mchungaji Mwenyeji, Innocent Ikechukwu amesema kuwa wananchi wajitokeze ili kupata maada mbalimbali za ukombozi na mafanikio.

Amesema huduma zitatolewa kwa siku tatu kuanzia leo Jumanne saa 11:00 jioni hadi alhamisi ambapo wahapingani kabisa na muda wa kazi hapa nchini kutokana na muda huo watu wengi watakuwa wametoka makazini.

Huduma hiyo itatolewa kwa lengo la kusaidia wanachi wenye matatizo mbalimbali, ili kupata upanyaji na kumtumaini Mungu,pamoja na Ukombozi na Mafanikio ambapo wanawaalika watu mbalimbali kuhudhulia mkutano huo ambapo mtoa maada katika siku tatu mfululizo ili kujipatia huduma za ukombozi na mafanikio.
 Mkuu wa Kanisa hilo, Dk. Enoch Aminu kutoka nchini Ghana akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kuwasili katika Kanisa la Moto halisi (Pure Fire miracles Ministries International') lilopo Tabata Segerea kwa Bibi jijini Dar es Salaam.
 Mchungaji Mwenyeji, Innocent Ikechukwuakizungumza wakati wa kumkaribisha  Mkuu wa Kanisa hilo, Dk. Enoch Aminu kutoka nchini Ghana mara baada alipo wasili kanisani hapo jijinio Dar es Salaam leo.
Pia amemshukuru kwa kuitikia wito wake kuja hapa nchini kutoa huduma ya neno la Mungu pamoja na ukombozi wa Mafanikio ya wanajamii watakao hudhuria katika huduma kanisani hapo.
Baadhi ya waumini wa Kanisa la Moto halisi (Pure Fire miracles Ministries International') lilopo Tabata Segerea kwa Bibi wakimuaga Mkuu wa Kanisa hilo, Dk. Enoch Aminu kutoka nchini Ghana mara baada ya kufika na kuongea na waumini hao.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...