WATAALAM wa afya katika kituo cha Maneromango kilichopo wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani wamefurahishwa kwa juhudi ya serikali ya awamu ya tano ya kuweka mkakati wa kukarabati kituo chao cha Afya.

Furaha ya wataalam hao wa Afya ilijitokeza wakati wa ziara za kikazi za Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo alipotembelea kituoni hapo kukagua maendeleo ya utoaji wa huduma za afya.

Wataalam hao wamesema kwasasa wanafanya kazi katika mazingira magumu kutokana na changamoto kubwa ya miundombinu.Kituo hicho kwasasa hakina chumba cha upasuaji, wodi za wagonjwa sambamba na ukosefu wa jengo Maalum la maabara.Kutokana na hali hiyo, Serikali imeamua kuwasaidia wananchi wa maeneo hayo kwa kuwajengea miundombinu ya jengo la upasuaji, maabara, nyumba ya watumishi.

Pia ujenzi wa miundombinu mingine unafanywa kwa fedha za ufadhili kutoka serikali ya Canada na tayari serikali inatarajia kupeleka Sh.milioni 500 kuanza ujenzi wa miundombinu hiyo. 

Akizungumza na wataalam hao, Naibu waziri jafo amebainisha kwamba changamoto ya miundombinu ya afya imekuwa kubwa ndio maana serikali imeamua kuanza kufanya ujenzi wa vyumba vya upasuaji na uimarishaji wa vituo vya afya zaidi ya 150 hapa nchini ili kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto.

Jafo amewaambia wataalam na wagonjwa waliokuwepo kituoni hapo kwamba serikali ya awamu ya tano imejipanga kuimarisha sekta ya afya hapa nchini.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kisarawe Hamisi Dikupatile na Mganga Mkuu wa wilaya Elizabeth na viongozi wengine katika ukaguzi wa kituo cha Afya Maneromango.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na viongozi mbalimbali wa wilaya ya kisarawe katika ukaguzi wa utoaji huduma za afya kwenye Kituo cha Afya Maneromango.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na wataalam wa Afya na wagonjwa katika kituo cha Afya Maneromango.
Baadhi ya wagonjwa wakisubiri kupata huduma za afya katika kituo cha Afya Maneromango.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...