Makamu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amkutana na kufanya mazungumzo na
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Bi. Bella Bird, Ikulu jijini
Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais na Mkurugenzi huyo walizungumzia masuala mbalimbali ya Lishe
kwa akina Mama na namna ukosefu wa lishe bora unavyopelekea vifo vya
akina mama na watoto wakati na baada ya kujifungua.
Aidha wamesisitiza suala la Elimu ya Lishe Bora kwa wakina mama hao ili kukabiliana na tatizo.
Makamu
wa Rais aliishukuru Benki ya Dunia kwa kuwasaidia wakina mama wa
Kitanzania na kuitaka iendelee kufanya hivyo hasa wakati huu ambapo nchi
inaenda kwenye uchumi wa viwanda.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Bi. Bella Bird mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam. (Picha na Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Bi. Bella Bird ambaye alimtembelea Makamu wa Rais ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam. (Picha na Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Bi. Bella Bird ambaye alimtembelea Makamu wa Rais ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam. (Picha na Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkaribisha ofisini kwake Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Bi. Bella Bird. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...