Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaambia washtakiwa sita wanaodaiwa kujihusisha na biashara ya meno ya tembo  akiwemo mfanyabiashara Yusuf Yusuf (34) maarufu ‘Mpemba’, kuelekeza lawama zao juu ya upelelezi kuchelewa kukamilika kwa mawakili wanaowatetea siyo wa Serikali tu.

Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amesema hayo mapema leo asubuhi wakati kesi hiyo ya uhujumu uchumi ilipofika kwa ajili ya kutajwa ambapo Wakili Wa serikali alidai jalada. 

Wakili Wa Serikali Elia Athanas alidai kuwa taarifa walizopeleka Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ambazo awali zilikosewa, walizifanyia marekebisho lakini bado hazijarudishwa ili waweze kuwasomea washtakiwa maelezo ya mashahidi (Committal.)

Hata hivyo, washtakiwa wamelalamika na kudai kuwa kila wakija wanaambiwa jalada halipo, ndipo hakimu akawashauri wawalalamikie pia mawakili wanaowatetea na siyo wa upande wa serikali tu kwani na wao wamekuwa wakikaa kimya tu. 

"Muwe mnawalalamikia na mawakili wenu pia siyo wa Serikali tu, ili hii kesi iweze kwenda kwa haraka", amesema Simba

Kesi hiyo imahirishwa hadi Octoba 10 kwa ajili ya kutajwa

Mbali na mpemba, washtakiwa ni Charles Mrutu (37) mkazi wa Mlimba, Morogoro, Benedict Kungwa (40) mkazi wa Mbagala Chamazi, Jumanne Chima (30) mkazi wa Mbezi, Ahmed Nyagongo (33) dereva na Pius Kulagwa (46) 

Wote wanakabiliwa na mashitaka manne ya kujihusisha na biashara ya meno ya tembo yenye thamani ya Sh milioni 785.6.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...