Na Frank Mvungi-MAELEZO, Dodoma.
Serikali imetoa takribani Shilingi Bilioni 21 kwa ajili ya kuboresha shule 85
za Kata hapa nchini ili ziwe na Kidato cha Tano na Sita hali itakayoongeza
ubora wa kiwango cha elimu na kuimarishwa kwa miundombinu.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe. Selemani Jafo
wakati wa kipindi cha TUNATEKELEZA kinachorushwa na Shirika la
Utangazaji Tanzania (TBC) siku za Jumatatu na Alhamisi.
Akifafanua Waziri Jafo amesema kuwa dhamira ya Serikalini katika
kuboresha sekta ya elimu ambapo kila mwezi imekuwa ikitoa takribani
Bilioni 23 zinazotumika kugharimia elimu bure hali inayochochea
kuongezeka kwa wanafunzi wanaojiunga katika shule za msingi na
Sekondari .
“Tumejenga madarasa mengi na vyoo vingi ili kuendana na kasi ya udahili
wa wanafunzi na pia tutahakikisha kuwa kuna kuwa na uwiano katika
mgawanyo wa walimu katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Aliongeza kuwa Serikali katika kuboresha huduma za Afya imeshapeleka
fedha katika vituo 172 kote nchini ili kuboresha huduma zinazotolewa na
pia watumishi katika sekta hiyo wataajiriwa kwa kuzingatia mahitaji
kutokana na nafasi zilizoachwa wazi baada ya zoezi la ukaguzi wa vyeti
feki.
Aidha Waziri Jafo aliwataka Viongozi wote katika Mikoa na Halmashauri
kusimamia vizuri miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali
katika maeneo yao ili thamani halisi ya fedha zilizowekezwa ionekane.
“Nawasihi watanzania walipe kodi kwa kuwa fedha zinazotokana na kodi
ndizo zinazotumika kutekeleza miradi ya maendeleo na ni matumaini
yangu kuwa maelekezo niliyotoa kwa wakurugenzi kuhusu ukusanyaji wa
mapato yatazingatiwa na watasimamia kazi hiyo vyema na kubuni vyanzo
vipya vya mapato”, alisisitiza Jafo.
Aidha Waziri Jafo amewataka watumishi wa Wizara hiyo kuacha kufanya
kazi kwa mazoea kwa kuwa hadi sasa watumishi zaidi ya 300
wameshachukuliwa hatua mbalimbali za kinidhamu kwa kushindwa
kutimiza wajibu wao.
Kwa upande wa sekta ya Viwanda amebainisha kuwa wamejipanga vyema
kutekeleza dhana ya ujenzi wa uchumi wa viwanda kwa kutenga maeneo
maalum ya uwekezaji katika Halamashauri na Mikoa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...