BENKI ya CRDB tawi la Kariakoo lasherekea wiki ya huduma kwa wateja ambayo inafanyika kila mwaka kwa wiki nzima kuanzia leo Oktoba 2 hadi Oktoba 6,2017.

Akizungumza katika uzinduzi wa wiki ya Huduma kwa wateja, Meneja wa benki ya CRDB tawi la Kariakoo, Diana Mtalo jijini Dar es Salaam leo amesema wiki hii ni wiki ya huduma kwa wateja na ni wiki ya kuwahudumia wateja pamoja na kuwahamasisha wateja wajitokeze kufungua akaunti katika benki hiyo katika tawi la Kariakakoo jijini Dar es Salaam.

Amesema wateja ambao hawana akaunti katika benki hiyo waende wakafungue ili kuweza kujipatia huduma kedekede zilizopo katika benki hiyo ikiwa pamoja na kujipatia mikopo.
Meneja wa benki ya CRDB tawi la Kariakoo, Diana Mtalo akizungumza na wateja wa Benki ya CRDB tawi la Kariakoo jijini Dar es Salaam na kuwashukuru pamoja na kuwaomba kufungua akaunti za benki katika Tawi hilo kwani wanatoa mikopo mbalimbali katika tawi hilo. Wiki ya Huduma kwa mteja huadhimishwa kila mwaka kwaajili kusherekea pamoja na kuwahudumia wateja wao inavyopaswa.
Baadhi ya Wateja wa Benki ya CRDB tawi la Kariakoo wakifungua Shampeini kwaajili ya kusherekea pamoja wiki ya huduma kwa wateja ambalo huadhimishwa kila mwaka. 
Meneja wa benki ya CRDB tawi la Kariakoo, Diana Mtalo pamoja na wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Kariakoo wakigonganisha glasi za shampeni kwaajili ya kudherekea wiki ya huduma kwa mteja ambayo huadhimishwa kila mwaka.
Wateja wa benki ya CRDB tawi la Kariakoo wakilishwa keki ikiwa ni kuadhimisha ufunguzi wa wiki ya huduma kwa wateja jijini Dar es Salaam leo.
Wateja na wafanyakazi wa beki ya CRDB tawi la Kariakoo wakiwa katika picha ya pamoja ikiwa ni kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila mwaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...