MKUU wa Wilaya ya Ubungo,Kisare Makore amewataka wamiliki wa vyombo vya moto kuzingatia sheria za barabarani ili kuepuka ajali zinazosababishwa na madereva wazembe na kuwataka kufanya kazi kwa kuzingatia sheria zilizopo.

Mkuu huyo wa Wilaya ameyasema hayo wakati wa uwekaji saini wa mkataba kati ya Chama Cha Madereva na wamiliki pikipiki mkoa wa Dar es Salaam (CMPD) na Kampuni ya Tanzania Motorcycle and Bajaji Association (TAMOBA)

Kwaajili ya kuzisajili pikipiki na bajaji katika mfumo wa Tanzania tracking technology and security monitoring system utakaowawezesha kujua pikipiki iliyoibiwa ipo eneo gani na kuweza kupatikana kwa haraka zaidi.

Aidha Makore amesema madereva wa pikipiki na bajaji walikuwa na wasiwasi wa kuibiwa vyombo vyao hivyo ila TAMOBA imeleta usalama mzuri kisasa kwa kuwa madereva hao watafanya kazi zao wakiwa hawana wasiwasi wa kuibiwa pikipiki zao na mali zao wawapo katika majukumu yao hayo pamoja na abiria wao.

Kwaupande wake Afisa Utumishi wa TAMOBA,Erasto Lahi amesema kwamba kampuni hiyo inatoza Shilingi mia moja kwa siku kwaajili ya kulinda pikipiki na bajaji

“Mtu aliye katika mfumo huu atapata msaada wa kulindwa muda wote masaa 24, hivyo mmiliki wa chombo muda wowote akihitaji taarifa za chombo kilipo, kilipopita na kinapoelekea atazipata, pia mfumo huu utaunganishwa na Jeshi la Polisi moja kwa moja ili kuharakisha zaidi huduma za kiusalama”alisema Lahi.


Mkuu wa Wilaya ya Ubungo,Kisare Makore (wapili kushoto) kwakushirikiana na viongozi mbalimbli akizindua ofisi za Chama Cha Madereva na wamiliki pikipiki mkoa wa Dar es Salaam (CMPD)
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo,Kisare Makore akizungumza katika hafla ya kusaini makubaliano ya usajili wa pikipiki na bajaji katika mfumo wa Tanzania tracking technology and security monitoring system utakaowawezesha kujua pikipiki iliyoibiwa ipo eneo gani leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TAMOBA,Joseph Kimisha akizungumza baada ya kusaini makubalino na Chama Cha Madereva na wamiliki pikipiki mkoa wa Dar es Salaam (CMPD) kwajili ya usajili wa pikipiki na bajaji katika mfumo wa Tanzania tracking technology and security monitoring system.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TAMOBA,Joseph Kimisha na Mwenyekiti wa Chama cha Madereva na wamiliki pikipiki mkoa wa Dar es Salaam (CMPD),Michael Massawe wakisani hati za makubaliano kwajili ya usajili wa pikipiki na bajaji katika mfumo wa Tanzania tracking technology and security monitoring system.

 Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...