Mhifadhi wa Wanyama Pori wa Selous kanda ya Matambwe, Gregory Kalokole akitoa maelezo machache juu ya hifadhi ya Selous. PORI la akiba la Selous ni moja kati ya hifadhi zenye utajiri wa vivutio adimu vya utalii na ambavyo vinapaswa kutangazwa zaidi kwa ajili ya watalii wa ndani na wa nje. 

 Selous ni pori la akiba lenye ukubwa wa kilometa za mraba 54,000 likijumuisha maeneo ya ardhi oevu, misitu ya miombo, tambarare, nyasi za kuvutia, maziwa na mito inayotiririka, vyote vikifanya vivutio vya aina yake mbali na wanyama wa aina mbalimbali. Pori hili la akiba la Selous lilianzishwa mwaka 1896 na Wajerumani likiwa ni pori la kwanza kutengwa kwa ajili ya uhifadhi wa wanyamapori katika Bara la Afrika na la pili duniani kwa ukubwa baada ya hifadhi ya pori la Marekani ambalo linaitwa Yellowstone. 

Pori hili limegawanyika katika kanda 8 kiutawala. Umaarufu wa Selous si katika wanyama pekee ambao ndiyo kivutio kikubwa cha utalii wa uwindaji, utafiti umebaini kuwa katika eneo la Selous kuna utajiri mkubwa wa maliasili ya mimea ambayo ikitambuliwa na kutangazwa inaweza kuwa kivutio adimu na cha kipekee cha kitalii.
 Wakisoma ramani mbali mbali inayoonyesha hifadhi hiyo.
 Moja ya ramani.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana waliosoma nchini China (CAAT), Dkt. Liggyla Vumilia akizungumza machache na Mhifadhi wa Wanyama Pori wa Selous kanda ya Matambwe, Gregory Kalokole.
 Moja ya wanyama wanaopatikana katika hifadhi ya Selous.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...