Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeipiga kalenda hadi Desemba 15/2017 kesi ya uhujumu uchumi na kusababisha hasara ya USD 3.7 milioni ambayo ni sawa na bilioni nane. inayowakabili vigogo wanne wa Kampuni ya Six Telecoms Limited na kampuni yenyewe.

Hatua hiyo imekuja baada ya wakili wa upande wa mashitaka, Jackline Nyantori kuieleza mahakama kuwa, upelelezi dhidi ya kesi hiyo bado haujakamilika na wanajitahidi kukamilisha mapema.

Wakili wa utetezi Masumbuko Lamwai akizungumza kuhusu upelelezi amedai, kesi wanayokabiliwa nayo washtakiwa siyo mpya, kwani ilishafikishwa mahakamani hapo kama kesi ya uhujumu uchumi Namba 2 ya mwaka 2016.

Amedai, upande wa mashtaka wanazo taarifa zote juu ya shauli hilo sababu mashtaka wanayoshtakiwa nayo ni juu tarrif za simu ambazo ni electronic na ziko recodedi hivyo hamna ushahidi wowote ambao bado haujakamilika.

"Wateja wetu wana umri mkubwa wametumikia nchi hii kwa muda mrefu, wanaambiwa upelelezi bado wakati mambo yote yako wazi, hii ni kuonesha kuwa hawana nia nzuri nao, wanataka tu kuwaweka ndani, tunaomba waambiwe wakamilishe upelelezi twenda mahakama kuu kusikiliza kesi.

Kufuatia hoja hizo, Wakili Nyantori amedai, siyo kweli kwamba hiyo kesi ni ya pili, kesi ya uhujumu uchumi Namba 2/2016 washtakiwa wa zamani ambao wapo kwenye kesi hii mpya ni wawili tu lakini hii mpya wako wanne, pia katika kesi hiyo kulikuwa na mashtaka mawili na hii mpya mashtaka ni matano, kwa hiyo ni kesi mbili tofauti. Tutajitahidi kukamilisha upelelezi.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 15 mwaka huu, washtakiwa wamerudishwa rumande.Washtakiwa katika kesi hiyo ni Mhandisi na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Six telecoms, Hafidhi Shamte, Mfanyabiashara na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Peter Noni, Mwanasheria na Mhadhiri na Mkurugenzi wa hiyo kampuni Dr ,Ringo Tenga, Mkuu wa fedha wa kampuni hiyo Noel Chacha na Kampuni ya Six Telecoms Limited. 

Wote kwa pamoja wanadaiwa kuhujumu miundombinu ya mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA), kwa kutoza garama chini ya kiwango, kushindwa kulipa ada za udhibiti na kutakatisha 3,282,741.12 

Pia washtakiwa hao wanadaiwa kuisababishia TCRA hasara ya USD 3,748,751.22, sawa na Sh 8 bilioni za kitanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...