Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Mfanyabiashara James Rugemarila anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha amedai mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa unahitajika ushirikiano baina yake na upande wa mashtaka ili kumbaini mwizi wa Bil 309 za serikali wanazodaiwa kuiba.

Katika kesi hiyo, Rugemarila, anashtakiwa pamoja na mmiliki wa IPTL, Harbinder Singh Sethi ambapo wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi likiwemo la utakatisha fedha na kuisababisha serikali hasara ya USD 22, 198,544.60 na Bil 309.

Rugemarila amedai hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Mwendesha Mashtaka kutoka Takukuru, Leornad Swai kuieleza mahakama kuwa kesi leo imekuja kwa kutajwa na upelelezi bado haujakamilika.

Rugemarila alidai upelelezi wa tuhuma zao ulianza tangu 2014 na sio miezi sita iliyopita kama alivyoeleza.Amedai kuwa anahitaji apate ushirikiano kutoka kwa upande wa Jamhuri ili wamjue na kumtaja ni nani mwizi wa Bil.309 za serikali.Aidha amedai kuwa hajawahi kupata nafasi ya kuzungumza na mawakili wake tangu alipotoka mahakamani hapo tarehe iliyopita.

"Nashindwa kupata ushauri, wala sijui nini kinaendelea kuhusu kesi yangu, hivyo angalau naomba waruhusiwe mawakili angalau wawili badala ya 10 ili wawe wananielezea kuhusu ilipofikia hii kesi,".Awali kabla ya kutoa hoja hizo, Wakili wa utetezi Balomi alidai kuwa suala la upelelezi katika kesi hiyo linachelewesha, huku ikizingatiwa linakiuka misingi ya haki ya kikatiba kwa washtakiwa.

" Ni miezi 6 sasa, tunaambiwa upelelezi haujakamilika, Wakili wa serikali anashindwa hata kutuambia umefikia wapi na umebaki muda gani kukamilika,".Pia Wakili Balomi amedai kuwa hali ya washtakiwa kiafya sio nzuri hasa Seth, hivyo upelelezi ukamilishwe kwa haraka ama wawe wanaelezwa hatua ulipofikia.Akijibu hoja hizo Wakili Swai alidai kuwa, upande wa utetezi ndio umekuwa ukikwamisha mchakato wa upelelezi kwani wamekuwa wakinyimwa baadhi ya nyaraka.

Swai aliongeza kudai, kuchelewa kwa upelelezi huo pia kunasababishwa na ushahidi mwingine kuwepo nje ya nchi.Kesi hiyo imeahirishwa hadi December 22, 2017 upande wa mashtaka umetakiwa kukamilisha upelelezi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...