Na Joel Maduka,Geita

Mwanasheria Mkuu wa Mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM) David Nzarigo amekamatwa na serikali baada ya kudaiwa kukutwa na nyaraka za serikali .

Mwanasheria huyo amekamatwa kwa amri ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh,Kangi Lugola alipotembelea Mgodi huo ambapo pamoja na mambo mengine amebaini mgodi huo kuwa unaendesha shughuli zake bila kufuata sheria ya mazingira .

Akiwa katika katika ziara ya kikazi ya siku mbili Wilayani Geita,Mhe.Kangi Lugola ameagiza kukamatwa kwa mwanasheria huyo baada ya kudaiwa kukutwa na nyaraka za serikali ambazo hazijawa rasmi kutumika kutoka taasisi ya wakala wa utafiti wa jiolojia Tanzania(GST).

Hata hivyo katika hali isiyo ya kawaida na bila kutarajiwa.Mwanasheria huyo aliyekuwa akiukingia kifua mgodi huo ili usikumbane na rungu la fidia ya uharibifu wa kimazingira kama sheria inavyotamka, alijikuta akimweleza Naibu Waziri kuwa anayo ripoti ya GST aliyodai haijaeleza iwapo mgodi huo unahusika moja kwa moja kwenye uharibifu hivyo mgodi huo usibebeshwe mzigo huo.

Kutokana na hali hiyo,Naibu Waziri Lugola aliomba apatiwe ripoti hiyo ili ajiridhishe,lakini mwanasheria huyo akijibu kwa kujiamnini alimtaka kiongozi huyo wa juu kutumia mbinu zake kuipata Serikalini, lakini yeye hawezi kutoa nyaraka ya serikali, jambo lililomkasirisha Naibu Waziri wa Muungano na Mazingira na kutoa agizo la kukamatwa mara moja.

Mwanasheria Mkuu wa Mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM) David Nzarigo akipandishwa kwenye gari ya Polisi Baada ya agizo la Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh,Kangi Lugola. 
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh,Kangi Lugola akipokea taarifa ya shughuli zinazofanywa na Mgodi huo. 
Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akitazama baadhi ya nyaraka wakati ambapo Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh,Kangi Lugola. 
Mwanasheria Mkuu wa Mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM) David Nzarigo akipelekwa kwenye gari la polisi na askali baada ya agizo la Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh,Kangi Lugola. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...