Taasisi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na masuala ya kifedha ya Tanzania Mortage Refinance Company (TMRC) imekabidhi msaada wa shilingi milioni nane kwa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kuwezesha matibabu ya moyo kwa watoto wanne.

Watoto hao watafanyiwa upasuaji wa moyo wa kuziba matundu na wengine kutibiwa mishipa ya damu ambayo haipitishi damu vizuri katika moyo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkurugenzi wa TMRC Oscar Mgaya alisema wameguswa kuchangia fedha hizo ili kuokoa maisha ya watoto hao wenye matatzo ya moyo ambao ni Taifa la kesho.

“Tumetoa shilingi millioni nane kwa ajili ya upasuaji wa kutibu magonjwa ya moyo kwa watoto wanne, tumeguswa kutoa fedha hizi ikizingatiwa watoto wengi ni wadogo hawajafikisha hata miaka mitano na watalaam wanaeleza ikiwa hawatapatiwa matibabu hasa ya upasuaji kwa wakati muafaka wataweza kupoteza maisha”,.

“Moyo ni kiungo cha muhimu sana katika mwili wa binadamu, unaweza kukosa mguu au mkono ukaishi lakini siyo moyo, binadamu akikosa moyo hawezi kuishi”, alisema.Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi aliishukuru Taasisi ya TMRC kwa kutoa fedha hizo ambazo zitaokoa maisha ya watoto wanne wanaosumbuliwa na matatizo ya moyo.

Prof. Janabi alitoa rai kwa Taasisi zingine kuiga mfano na kuendelea kujitokeza kufadhili matibabu ya watoto ambao bado wanasubiri kufanyiwa upasuaji wa moyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taaasisi ya Moyo Jakaya Kikwete(JKCI) Prof. Mohamed Janabi na Mkurugenzi wa Taasisi ya kifedha ya Tanzania Mortage Refinance Company(TMRC) Oscar Mgaya wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wenye matatizo ya Moyo na wazazi wao wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya mfano wa hundi ya shilingi milioni nane ambayo wamezitoa kwa ajili ya matibabu ya watoto hao.
Mkurugenzi wa Taasisi ya kifedha ya Tanzania Mortage Refinance Company(TMRC) Oscar Mgaya akiwakabidhi wazazi wa watoto wenye matatizo ya Moyo mfano wa hundi ya shilingi milioni nane ambazo zimetolea na Taasisi hiyo kwa ajili ya matibabu ya watoto wanne.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taaasisi ya Moyo Jakaya Kikwete(JKCI) Prof. Mohamed Janabi na Mkurugenzi wa Taasisi ya kifedha ya Tanzania Mortage Refinance (TMRC) Oscar Mgaya wakizungumza baada ya kumaliza makabidhiano ya hundi ya shilingi million nane kwa ajili ya kuwezesha matibabu ya moyo kwa watoto wanne .Picha na JKCI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...