Na Veronica Simba – Dodoma
Waziri
wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amekagua maendeleo ya utekelezaji wa
Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) katika Wilaya za Kongwa
na Kondoa mkoani Dodoma.
Katika
ziara hiyo ya siku moja iliyofanyika Jumatatu Desemba 11, 2017, Waziri
Kalemani aliwasisitiza viongozi wa Halmashauri ambako Mradi wa REA III
unapita, kuhakikisha wanatenga fedha kwa ajili ya kuunganisha umeme
hususan katika Taasisi mbalimbali za umma.
“Siyo
vema Taasisi muhimu za umma zikaendelea kukosa umeme kwa kutokuwa na
fedha hivyo kuwatesa wananchi. Hakikisheni mnatenga fedha kwa shughuli
hiyo muhimu.”
Aidha,
alibainisha kuwa, maeneo yanayopewa kipaumbele katika Mradi wa REA III
ni Taasisi zote za umma ili kuhakikisha zinatoa huduma bora kwa
wananchi.
Pia,
aliwataka wakandarasi wanaotekeleza Mradi huo katika maeneo mbalimbali
nchini, kukutana na viongozi wa maeneo husika wakiwemo wabunge ili
wapewe mwongozo wa sehemu muhimu za kipaumbele zinazotakiwa
kuunganishiwa umeme.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (aliyeshika kipaza sauti) akiwasalimu wananchi wa Kijiji cha Pembamoto, Wilaya ya Kongwa, mkoani Dodoma, alipofanya ziara kukagua utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III)
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) akimkabidhi Spika wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai, kifaa kinachotumika kuunganisha umeme katika nyumba pasipo kutandaza nyaya, kijulikanacho kama UMETA. Waziri alitoa kifaa hicho kama zawadi kwa baadhi ya wazee katika Kijiji cha Makole, Wilaya ya Kongwa, wakati wa ziara yake kukagua utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini (REA III) pamoja na kuzungumza na wananchi.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (kulia), akifafanua jambo kwa Spika wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai (kushoto), alipokuwa katika ziara ya kazi jimboni humo kukagua utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III). Wengine pichani ni viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na wataalam kutoka wizarani, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...